WANACHAMA 2,565 WAJITOKEZA KUMDHAMINI DKT. MAGUFULI RUANGWA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia wakati mwanachama wa CCM, Jacob Masumbuko alipotia saini fomu ya kumdhamini, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili aweze kuteuliwa kuteuliwa tena kugombea urais. Zoezi hilo lilifanyika kwenye Ofisi ya CCM ya wilaya ya Rungwa, Juni 21, 2020. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa LIndi, Fadhili Juma.
Waziri Makuu, Kasim Majaliwa akishuhudia wakati wana CCM walipojitokeza  kujaza fomu za  kumdhamini Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili aweze kuteuliwa tena kugombea urais katika uchaguzi ujao. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi , Fadhili Juma.
Waziri Makuu, Kasim Majaliwa akishuhudia wakati wana CCM walipojitokeza  kujaza fomu za  kumdhamini Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili aweze kuteuliwa tena kugombea urais katika uchaguzi ujao. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi , Fadhili Juma
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudiwa wakati mwanachama wa CCM, Abdallah Milanzi  alipotia saini fomu za kumdhamini, Rais wa Dkt. John Pombe Magufuli katika ili aweze  kuteuliwa kugombee tena urais. Zoezi hilo lilifanyika kwenye Ofisi ya CCM ya wilaya ya Rungwa, Juni 21, 2020. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa LIndi, Fadhili Juma
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi fomu zenye majina , saini za wana CCM waliomdhamini Rais Dkt. John Magufuli ili aweze kugombea tena urais Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Ruangwa, Said Kaondo baada ya kumaliza  zoezi la  udhamini kwenye Ofisi ya CCM ya wilaya ya Ruangwa, Juni 21, 2020.Katikati ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Lindi, Fadhili Juma.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akigonganisha kiwiko na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Ruangwa, Said Kaondo baada ya kumkabidhi fomu zenye majina na saini za wana CCM waliomdhamini Rais Dkt. John Magufuli ili aweze kugombea tena urais. Tukio hilo lilifanyika  kwenye Ofisi ya CCM ya wilaya ya Ruangwa, Juni 21, 2020. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Lindi, Fadhili Juma.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
…………………………………………………………………………………..
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameongoza wanachama 314 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Ruangwa, Lindi katika kujaza fomu za kumdhamini Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili aweze kuteuliwa kugombea tena nafasi ya urais.
Idadi hiyo inafanya jumla ya wanachama waliojitokeza kumdhamini Rais Dkt. Magufuli katika wilaya hiyo kufikia 2,565 baada ya wanachama wengine 2,251 kujaza fomu hizo jana (Jumamosi, Juni 20, 2020) na kumdhamini kiongozi huyo.
Waziri Mkuu ameongoza wanachama hao wa CCM leo (Jumapili, Juni 21, 2020) katika ofisi za CCM wilayani Ruangwa. Amewasihi wananchi hao waendelee kuwa na imani na Rais Dkt. Magufuli pamoja na Serikali anayoiongoza.
“Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametekeleza ahadi zote alizoziahidi ikiwemo ya kuwatumikia Watanzania wote hasa wanyonge. Amewatumikia Watanzania wote bila ya kujali itikadi zao za kisiasa na hata za kidini. Nawapongeza wana CCM wenzangu mliojitokeza kumdhamini rais wetu.”
Waziri Mkuu ameongeza kuwa “Kitendo mlichokifanya leo kinaonyesha shukrani kubwa kwa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye wakati wote ameonesha mapenzi makubwa kwetu pamoja na Watanzania wote kwa ujumla.”
Amesema kwa sasa wilaya ya Ruangwa imepata mabadiliko makubwa kimaendeleo ambayo hapo awali hayakuwepo kama nishati ya umeme, maji ambayo kwa sasa kila kijiji kina kisima, shule za msingi katika kila kijiji na sekondari kwenye kata zote pamoja na barabara za lami katika mitaa ya mji wa Ruangwa.” Haya yote ni Dkt. Mgufuli.”
Kwa uapande wake, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi, Fadhili Juma amesema wanaCCM wa mkoa huo wapo bega kwa bega na Rais Dkt. Magufuli na kwamba watahakikisha anapata kura nyingi katika uchaguzi ujao.
Awali, Waziri Mkuu aliwashukuru WanaRuangwa wote kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chote cha miaka mitano ambao ulimuwezesha kutekeleza majukumu yake ya kuwaletea maendeleo kwa ufanisi mkubwa.

No comments: