WALEMAVU WAMKARIBISHA RASMI TUNDU LISSU WAMWAMBIA KURA ZAO ZOTE KWA JPM

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walemavu kupitiaChama Cha Mapinduzi(CCM)Peter Sarungi(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 21 ,2020 jijini Dar es Salaam kuhusu tamko lao kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.Kulia ni Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo John Mlabu.
 Kulia ni Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo John Mlabu(kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walemavu kupitiaChama Cha Mapinduzi(CCM)Peter Sarungi.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walemavu kupitiaChama Cha Mapinduzi(CCM)Peter Sarungi(kulia) akimkaribisha rasmi kada wa Chadema Tundu Lissu kwenye jumuiya ya walemavu huku akitumia nafasi hiyo kumtaka kuungana nao katika uchaguzi mkuu mwaka huu kwa kumchagua Rais Dk.John Magufuli ili waendelee kunufaika na mambo mazuri yanayofanywa na Dk.Magufuli. 

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walemavu kutoka Chama Cha Mapinduzi(CCM)Peter Sarungi(aliyevaa kofia nyeusi)akiwa na wajumbe wengine wa jumuiya hiyo wakiangalia sehemu ya hotuba ya Mwenyekiti huyo baada ya kumalizika kwa mkutano kati yao na waandishi wa habari.
 
Wajumbe wa jumuiya hiyo ya CCM ya Watu wenye ulemavu Charles Temba(kushoto) na Lameck Samson wakifuatilia kwa makini mkutano huo.
 
Mjumbe wa jumuiya hiyo Hamza Waritu akiwa makini kusikiliza hotuba ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walemavu CCM wakati akizungumza na waandishi wahabari leo Juni 21,2020 jijini Dar es Salaam.
 
Mmoja wa wajumbe wa jumuiya hiyo Ashura Narino akifuatilia mkutano huo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walemavu kupitiaChama Cha Mapinduzi(CCM)Peter Sarungi(kushoto), Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo John Mlabu(katikati) na Mjumbe wa jumuiya hiyo Charles Temba wakiwa makini kusikiliza maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano huo uliofanyika leo Juni 21,2020 jijini Dar es Salaam.

Na Said Mwishehe,Michuzi TV 

JUMUIYA ya Walemavu wa Chama Cha kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) wamemkaribisha rasmi Kada wa Chadema Tundu Lissu kujiunga na jumuiya hiyo baada ya kupata ulemavu huku wakitoa msimamo kuwa katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu walemavu wote kura kwa Rais Dk.John Magufuli.

Akizungumza leo Juni 21,2020 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walemavu kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) Peter Sarungi ameeleza wazi walemavu wote wanatakiwa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kuhakikisha anashinda na kwenye nafasi hiyo ya urais hakuna mtu mwenye ulemavu atajitokeza kumpinga Rais Magufuli zaidi ya kumpigia kura ya ndio.

Akifafanua zaidi kuhusu Lissu ambaye wamesikia ni miongoni mwa wanaotaka kuwania nafasi hiyo kwa tiketi ya Chadma, kwanza wanamkaribisha  rasmi kwenye jumuiya ya watu wenye ulamavu kwasababu uumbaji wa Mungu haujamalizika mpaka mtu aingie kaburini na ndio maana kuna msemo usemao hujafa hujaumbika.

"Kipindi cha nyuma tunajua Lissu hakuwa mtu mwenye ulamavu ,ameupatia ukubwani na hatujui kaupataje pate,  na tunajua siasa zake,tunajua aliyokuwa akisema na kutenda , na hakuna hata siku moja aliyowahi kuzungumzia mambo yanayohusu walemavu wa nchini kwetu.

"Kwa namna moja au nyingine sisi hatujawahi kusikia akituzungumzia kwa namna yoyote ile, aidha akiwa bungeni au kwa waandishi wa habari lakini kwa kuwa sasa naye ni mlemavu mwenzetu tunamkaribisha kwenye kundi letu.Tunachomuomba afuate miongozo ya jamii ya watu wenye ulamavu ambayo ipo na inafuatwa na waliopo kwa muda mrefu.

"Sisi walemavu wa muda mrefu ambao tumezaliwa nao tutamuelekeza namna ya kuheshimu na kufuata miongozo iliyopo ya watu wenye ulamavu, tunaweza kumuongoza apite wapi,atokee wapi, Kwa hiyo nadhani kwa ukaribisho huu tunamshauri kwamba Dk.John Magufuli anatosha kusemea watu watu wenye ulemavu, amekuwa akitutetea kwa vitendo  kabla ya kuwa Rais .Alipokuwa  Mbunge,alikuwa Waziri kote huko alikuwa pamoja nasi.

Ameongeza kuwa " Na amekuwa Rais leo hii tunaona mambo mengi ambayo yanahusu walemavu ameyaingiza kwenye mfumo wa nchi kiasi kwamba hata atakapoondoka tutakuwa tunajua hatma yetu, sasa haya mambo mazuri hata yeye Lissu atayafurahia.

"Hivyo ampe nafasi Dk.John Magufuli ili apeleke gurudumu hilo mbele la mambo mazuri ya walemavu  ili na sisi jamii ya Walemavu akiwemo na yeye Lissu ambaye ameingia kwenyw jumuiya yetu basi tuweze kunufaika wote kwa pamoja .Lissu akijitokeza kupambana na Dk.Magufuli walemavu hatutamuunga mkono."

 Wakati huo huo, Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya walemavu, amesema wanayofuraha kubwa  na kutoa pongezi kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk.Magufuli  kutokana na kuliongoza vema Taifa la Tanzania." Tumejitokeza hadharani kutoa pongezi kwa Rais Magufuli kwa hotuba nzuri aliyoitoa wakati akilifunga Bunge la 11 mjiji Dodoma.

"Katika hotuba yake amezungumzia mambo mengi mazuri  na yenye kuonesha mshikamano na umoja wa kitaifa kwa wabunge na Watanzania wote na sisi kama jamii ya Watanzania wenye ulemavu tunamshukuru Rais wetu kwa kuvielekeza vyama vya siasa kutujumuisha kwenye uchaguzi mkuu ujao.Rais Magufuli tunakuahidi tutajitokeza na tutakuunga mkono,"amesema.

Ameongeza kuwa kwa CCM imeweka utaratibu mzuri ambao umeondoa mianya ya rushwa ,hivyo ni nafasi ya watanzania kujitokeza kuwania udiwani na ubunge.

Hata hivyo amesema watu wenye ulemavu ambao wataonesha nia zao za kugombea kupitia vyama vyao vya siasa  na pengine kuteuliwa na kufanikiwa kushinda basi wachape kazi ili kuthibitisha uwezo wao mbele ya jamii na iwe ishara ya kuonesha kuwa wanaweza.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Walemavu CCM John Mlabu amesema watu wenye ulemavu wanaruhusiwa kugombea udiwani na ubunge na katika nafasi ya Rais hiyo ni ya Dk.Magufuli tu." Uchaguzi Mkuu kwa mwaka huu walemavu wote kura zetu kwa Rais Magufuli ,katika uongozi wake ameonesha mapenzi makubwa kwetu na hivyo nasi tutayaonesha kwa kumpa kura."

No comments: