RC SINGIDA AKAGUA NA KUTEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI MANYONI
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi (katikati) akivuta pazia kuashiria uzinduzi wa Bweni la Wanafunzi wa Kike wa Shule ya Sekondari ya Kinangali mkoani hapa jana. Kulia ni Katibu Tawala wa mkoa huo, Dk. Angelina Lutambi na kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Charles Fussi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi (wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Bweni la Wanafunzi wa Kike wa Shule ya Sekondari ya Kinangali. Kutoka kulia ni Katibu Tawala wa mkoa huo, Dk. Angelina Lutambi, Afisa Elimu Mkoa wa Singida, Mwalimu Nelasi Mulungu, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Charles Fussi, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Rahabu Solomoni na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Manyoni, Jumanne Makhanda.
Afisa Elimu Mkoa wa Singida, Mwalimu Nelasi Mulungu, akizungumza.
Bweni la Wavulana katika Shule ya Sekondari, Kinangali ambalo ujenzi wake umefikia hatua za mwisho.
Madarasa ya Shule ya Msingi Kinangali ambayo ujenzi wake umekamilika.
Mwakilishi wa Jeshi la Akiba Mkoa wa Singida katika ziara hiyo, Afisa Mteule Daraja II, Ramadhani Ngeri akizungumza.
Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Singida, Dismas Mosha, akizungumza.
Ziara ikiendelea.
Kiwanda cha kuchakata alizeti wilayani Manyoni ujenzi wake ukiendelea.
Mwonekano wa Bweni la Wanafunzi wa Kike wa Shule ya Sekondari ya Kinangali.
Safari ya ukaguzi wa miradi ikiendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi, akizungumza na Wafanyakazi wa Hospitali ya Wilaya Manyoni.
Wafanyakazi wa Hospitali ya Wilaya Manyoni wakiwa na viongozi mbalimbali wakati wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Nchimbi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi, akizungumza wakati akikagua ujenzi wa kiwanda cha kuchakata alizeti. Kulia ni Meneja wa kiwanda hicho. Mkuu wa MagerezaMkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi (ACP) Shaku Umba, akizungumza. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Manyoni Mjini, Magembe Machibula.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Furaha Mwakafwilwa akizungumza.
Wananchi wakiwa katika uzinduzi wa Bweni la Wanafunzi wa Kike wa Shule ya Sekondari ya Kinangali.
Afisa Elimu Wilaya ya Manyoni, Mkoa wa Singida, Ramlah Munisi, akizungumza.
Uzinduzi ukiendelea.
Moja ya mkorosho uliopandwa katika shamba la Korosho la Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) lenye jumla ya ekari 1,500 lililopo eneo la Sukamahela.
Wauguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Manyoni wakiwa kazini.
Na DottoMwaibale, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi amefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Manyoni.
Miradi aliyotembelea ni ukarabati wa wodi ya wazazi katika Hospitali ya wilaya hiyo, ujenzi wa Kiwanda cha kuchakata alizeti, ujenzi wa mabweni mawili katika Shule ya Sekondari ya Kinangali, ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika Shule ya Msingi Kinangali pamoja na kulikagua shamba la Korosho la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lenye jumla ya ekari 1,500 lililopo eneo la Sukamahela.
Akizungumza jana wakati akikagua ujenzi wa kiwanda cha kuchakata alizeti, Dk.Nchimbi aliwataka Makatibu Tawala wa mkoa huo wasikae maofisini badala yake watoke haraka waende kukagua maeneo ya uwekezaji yaliyotengwa kwenye halmashauri zao.
“RAS kwa ili tuna haja siku nyingine twende tukakague maeneo yaliyotengwa katika halmashauri zetu…taarifa za maandishi zinaeleza hayo maeneo yapo na kama yange kuwepo wewe husinge kwenda pale hukakosa hilo eneo kwa hiyo twende tuka kague hayo maeneo haraka sana.” alisema Nchimbi.
Nchimbi aliupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kuthubutu kukijenga na kusema anaona uchumi wa wilaya hiyo utabadilika kwa sababu mzunguko wake utaenda kwa kasi yenye thamani iliyo bora kutokana na uwepo wake.
Alisema suala la mafuta ni ajenda ya kitaifa na sio ajenda binafsi ya kiwanda hicho au Manyoni na Singida, kuwepo kwake mkoa huo utachangia kuipunguzia mzigo Serikali wa kutumia fedha za kigeni kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.
Dk. Nchimbi akizungumzia mradi wa ukarabati wa wodi ya wazazi alisema Serikali imetekeleza miradi mingi lakini kuna baadhi ya watu wamekuwa wakibeza hivyo wajue kuwepo kwa huduma ya uzazi na majengo hayo na vitanda inaonesha tafsiri pana ya uhai kwani hakuna taifa lolote duniani ambalo huwa linapanga kuwa ni taifa la miaka miwili au siku moja ni kwamba tunajijenga na kulihakikishia kwamba taifa letu siku moja linakuwa na uhai endelevu wa miaka mingi ijayo vizazi na vizazi.
”Rais wetu Dk.John Magufuli ameleta furaha na amani katika utumishi wetu kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo huu” alisema Nchimbi.
Akizindua mabweni ya shule hiyo Dk. Nchimbi alisema hali ya kusoma na idadi ya wasomi itaongezeka kwani watapata muda mzuri wa kujisomea pamoja na kumaliza changamoto ya maji na kupunguza ndoa za utotoni.
Akizungumzia mradi wa shamba la korosho alisema kilimo kinachofanyika katika shamba hilo ni cha pamoja kwani litakuwa shamba kubwa ambalo watu wengi watakuwa na visehemu wanavyolima.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida, Adili Elinipenda aliwaomba watumishi wa Umma mkoani hapa kuchangamkia fursa ya kupata shamba la korosho katika eneo hilo jambo litakalo wasaidia kupata kipato kitakachowafanya wasiweze kushawishika na kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa.
No comments: