Muhimbili yawashukuru wachangiaji Damu



Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi Hospitali ya Taifa Muhimbili -Mloganzila Dkt. Lulu Sakafu akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya uchangiaji damu duniani yenye kauli mbiu isemayo “damu salama, kwa wote” inayoadhimishwa Juni 14 kila mwaka
Afisa Uhamasishaji Damu Bw. John Bigambalae akiwaelezea wananchi umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kuchangia damu leo.
Baadhi ya wananchi wakichangia damu katika maadhimisho ya siku ya damu.
Viongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili katika picha ya pamoja na baadhi ya wachangiaji damu waliofika hospitalini hapa.
Mmoja kati ya wachangiaji damu wa mara kwa mara Bw. Clement Bocco akichangia mada wakati wa maadhimisho hayo.
Meneja wa Maabara MNH-Mloganzila Bi. Esuvat Moses akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi wa maadhimisho ya siku ya damu yaliyofanyika Mloganzila.
************************************


Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila hutumia unit 40 hadi 60 kutokana na mahitaji mbalimbali ya wagonjwa wanaofikishwa Hospitalini hapa.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi Hospitali ya Taifa Muhimbili -Mloganzila Dkt. Lulu Sakafu wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya uchangiaji damu duniani yenye kauli mbiu isemayo “damu salama, kwa wote” inayoadhimishwa Juni 14 kila mwaka iliyokwenda sambamba na kutoa shukrani kwa wachingiaji damu wa mara kwa mara.

“Kwa siku moja Hospitali inatumia chupa 40 hadi 60 ukilinganisha na kiwango cha ukusanyaji wa damu kwa siku ambao ni chupa 15 hadi 30 kwa siku kwa takwimu hii mahitaji ya damu bado ni makubwa”amesema Dkt Sakafu

Dkt. Sakafu amewashukuru wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakijitokeza kuchangia damu mara kwa mara kwa kuwa msaada huo umesaidia sana kuokoa maisha ya wamama wajawazito, wahanga wa ajali mbalimbali , wagonjwa wa saratani za damu na wengine wengi wenye mahitaji kama hayo

Amesema kuwa Kihistoria Hospitali ya Taifa Muhimbili ilikuwa ikitegemea mgao wa damu kutoka Kitengo cha Damu Salama cha Taifa (NBTS), lakini kutokana na ongezeko la uhitaji wa damu , Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto kwa kushauriana na uongozi wa mpango wa damu salama na uongozi wa Hospitali ya Muhimbili ulibariki mpango wa kuiwezesha timu ya kitengo cha damu salama Muhimbili kuweza kukusanya damu jijini Dare s salaam ili kukidhi mahitaji ya wagonjwa wote wa hospitali wanaohitaji damu.

Kwa upande wake Bw. Thomas Mkwiji ambaye ni mchangiaji damu wa mara kwa mara alishauri Kitengo cha damu salama Muhimbili kutoa elimu zaidi kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia damu ili watu wengi zaidi wajitokeze kuchangia damu kwa hiari.

No comments: