Aua wakwe zake (mme na mke) kwa tuhuma za ushirikina
Aua wakwe zake (mme na mke) kwa tuhuma za ushirikina
Na Amiri kilagalila,Njombe
Kijana aliyejulikana kwa jina la Patrick Ngailo mkazi wa Mlangali wilayani Ludewa mkoani Njombe,anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji ya wakwe zake (mme na mke) akiwatuhumu ni washirikina wanaomsababishia maradhi ya mara kwa mara.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema kijana huyo alitenda kosa hilo katika kijijji hicho June 8,2020 majira ya saa moja jioni lakini wananchi kwa kushirikiana na jeshi la polisi wamemkamata kijana huyo.
“Baaa ya kufanya maauaji haya huyu mtu alikimbia lakini wananchi walishilikiana na jeshi la polisi alikamtwa na sheria inafuata mkono wake”
Awali kamanda Issa alisema jeshi hilo limefanya uchunguzi na kubaini kuwa Ngailo alioa mtoto wa wazee hao lakini akapatwa na maradhi ya mara kwa mara na kuchukuwa uamuzi wa kwenda mkwa mganga alikoelezwa kuwa anapata maradhi kutokana na mke wake.
“Awali alioa mtoto wao baada ya kuoa mtoto huyo alienda kwa mganga kutokana na kumwa umwa na akajulishwa yeye anaumwa kwasbabu ya huyo mwanamke aliyemuoa akaamua kumuacha yule mwanamke,lakini cha ajabu kilichotokea alikuwa anaendelea kuumwa na alichokifanya aliamua kwenda kufanya mauaji ya mke na mume”alisema kamanda Issa
Aidha katika tukio jingine kamanda Hamis amesema lipo tukio jingine lililotokea hivi karibuni mkoani Njombe la kuuawa kwa mwanaume mmoja kutokana na kushambuliwa na vitu vyenye ncha kali akiwa amelala hali iliyofanya jeshi hilo kuwashikilia mama na watoto wa familia hiyo.
“Kuna tukio jingine la mauaji yenye utata ambalo baba na mama walilala katika nyumba moja lakini vyumba tofauti na asubuhi walipoamka baba alikuwa amefariki na kufariki kwenyewe kumetokana na kushambuliwa na vitu vyenye ncha kali,na hivi tunavyoonge mama na watoto wameshikiliwa kwa kuwa mauaji hayo yanaonekana yamefanywa na wanafamilia,jeshi la polisi linaenelea na uchunguzi na ukikamilika wahusika tutawafikisha kwenye vyombo vya sheria”alisema kamanda
Vile vile kamanda wa Polisi amesema jeshi hilo linawashikilia vijana wa mashambani waliomsababishia kifo kiongozi wao kutokana na kununua Sola huku vijana wake wakishindwa kuridhika.
“Huko maeneo ya mashambani kuna kiongozi wa Vibarua wa mashambani ambaye huwagawia mshahara wenzake lakini alinunua Sola ya kumulika mashambani bila wafanyakazi wenzake kuridhika,ukatokea ugomvi ukapeleka huyu kiongozi akafariki”alisema Issa
Kamanda wa polisi Hamisi Issa ametoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa
No comments: