WAWILI WASHIKILIWA NA POLISI KWA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI
Na.Vero Ignatus,Arusha
Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha linawashikilia Waandishi wawili raia wa nchi jirani ya Kenya kwa kosa la kuingia nchini bila kibali
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shana amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Clinton Isimbu( 22)kabila Mluya,mpiga picha wa Elimu Tv ya Kenya,mwingine ni Kaleria Shadrack(23)kabila mmeru ambaye pia ni mwandishi wa habari Elimu Tv ya nchini Kenya.
Kamanda Shana amesema watuhumiwa hao waliingia nchini kwa njia ya Panya,ambapo kwa Sasa wote wawili wamekabidhiwa kwa Idara ya Uhamiaji mkoa wa Arusha kwa hatua zaidi za kisheria.
Aidha watuhumiwa hao walikamatwa tarehe 16/5/2020 majira ya 13:30hrs maeneo ya mtaa wa kisongo kata ya Namanga,tarafa ya Longido.
No comments: