WANAOTUHUMIWA KWA MAKOSA 667 WAWATUHUMU MAWAKILI WA SERIKILI KUSEMA UONGO MAHAKAMANI

 
 Watuhumiwa wakitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.

MSHTAKIWA Yared Jonas anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  yenye mashtaka 667 likiwemo la wizi wa Umeme pamoja na wenzake wanne amedai kuwa hawakuwahi kutegemea kusikia mawakili wa serikali wanasema uongo mahakamani.

Mbali na Jonas, washtakiwa wengine ni Emilian Mlowe, Bashiru Ngella, Shakira Ngella na Mkama Maira.

Jonas amedai anashangaa kuona wanawabadirishia mashtaka na kuwapa mashtaka mapya kisha wanasema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Mshtakiwa amedai hayo leo Mei 18, 2020 wakati kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 42 ilipoitwa kwa ajili ya washtakiwa kusomewa mashtaka mapya baada ya mashtaka ya zamani kufutwa na mahakama kuwaachi huru kufuatia DPP kuwasilisha Nole Prosequi chini ya kifungu  cha 91 (1) cha makosa ya jinai (CPA) KU1wa DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yao.

Washtakiwa hao walikamatwa tena na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka 667 yakiwemo ya kula njama, wizi, kufanya udangangifu, utakatishaji fedha na kusababisha hasara kwa Tanesco ya zaidi ya Sh. Bilioni mbili.

Katika mashtaka mapya imedaiwa kati ya Januari 7 2014 na Julai 31 2015 jijini Dar es Salaa, washtakiwa hao kwa makusudi na kwa nia ya kutendakosa, walikula njama ya kutenda kosa la wizi.

Aidha imedaiwa kati ya Julai 31 2014 na Machi 31 2016 washtakiwa hao walijipatia kiasi cha sh. 2,746,485,546.63 huki wakijua kuwa  fedh hizo ni zao la kosa tangulizi la wizi.
Pia imedaiwa kati ya Julai Mosi 2014 na Machi 31 2016 huko katika ofisi za Tenesco za mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam washtakiwa hao kwa makusudi waliisababishia Tanesco hasara ya kiasi hicho za bilioni. 2.7.

Baada ya kusomwa kwa mashtaka hayo mshtakiwa Jonas alidai kesi yao hiyo ni ya muda mrefu, walikuwa nje kwa dhamana tangu mwaka 2014, na mwaka 2017 walifikishwa mahakamani na kuweka ndani kwa kuwa kesi yao haina dhamana.

"Mheshimwa, kesi hii imeishapita mikononi mwa Mahakimu wanne tofauti, mawakili wa serikali walishasema upelelezi umekamilika  na wanasubiri sahihi ya DPP ili watusomee commital kesi iwezi kwenda mahakama ya mafisadi leo wanabadirisha chaji halafu wanasema upelelezi bado, ebu muogopeni Mungu na sisi ni binadamu ni watanzania wenzenu  tuna watoto, tuna wazazi tuna familia, mnatoa kauli za uongo mbele ya mahakama.." analalamika Mshtakiwa Jonas 

" Mwenzetu mmoja alifariki toka Desemba mwaka jana lakini  leo ndio jina lake imefutwa mawakili wa serikali wanaongea uongo tulijua mahakamani ndio kuna uhakika wa kupata haki kumbe mawakili wa serikali ni waongo kila siku wanakuja wanadanganya hawana nia njema na sisi machoni pa Mungu wala mbele ya mahakama.

Akijibu hoja hizo wakili  wa serikali Easter  Martin Medai, taarifa wanazoleta mahakamani siyo za uongo, ni za kweli na zinapatikana kutokana na jinsi upelelezi wa kesi unavyoenda.

Hata Hivyo, Hakinu Issaya amewaeleza washtakiwa hao kuwa kesi hiyo ni mpya mbele yake na mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza wala kutoa dhamana. Kesi itatajwa tena Juni Mosi mwaka huu, washtakiwa wamerudishwa rumande.

No comments: