wananchi watakiwa kuelimishana kuhusu corona.
Na Woinde Shizza,ARUSHA
Chama Cha wafanyabiashara ( TCCIA)Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na Trade Mark East Africa na TRIAS kimegawa vifaa kinga vyenye thamani ya sh,mil. 4 kwenye masoko matatu katika jiji la Arusha kama njia Moja wapo ya kupambana na maambikizo ya ugonjwa hatari wa Corona na kuunga mkono jitihada za serikali dhidi ya ugonjwa huo.
Akikabidhi vifaa hivyo zikiwemo ndoo za maji ya kutiririka,vitakasa mikono na Barakao ,mwenyekiti wa TCCIA ,Wolter Maeda aliwataka wafanyabiashara katika masoko hayo kuhakikisha wanajikinga na Corona kwa kutumia vifaa hivyo.
Aliwakumbusha wafanyabiashara hao kuhakikisha wafanyabiashara zao katika mazingira salama ,ikiwemo kuosha mikono yao kwa sabuni kukaa umbali wa mita moja na kuvaa barakoa ili kujikinga na janga hilo .
"Nipende kuwasihi wafanyabiashara na kuwaambia ugonjwa huu upo na unaua kweli kweli ni vyema kuchukuwa taadhari na kuacha kupuuzia ushauri unaotolewa na idara ya afya ,hapa tu nikiangalia kunawafanyabiashara hawajavaa barakoa ,nimeona hawanawi mikono sasa niwaombe msifanye mzaa kwenye ugonjwa huu chukuweni taadhari "alibainisha Maeda
Naye Afisa Maendeleo ya Biashara wa TCCIA,Charles Makoi alisema kuwa masoko yaliyonufaika na msaada huo ni Kilombero,Samunge(Krokon) na Soko kuu ambapo wanufaika wa mpango huo ni wafanyabiashara wadogo(Machinga),Mama ntilie na wauzaji wa mbogambona na matunda.
Aliwasihi wananchi kuendelea kupeana elimu wao kwa wao nila kuopa na kuoneana aibu ili kuweza kuendelea kuwanusuru wale ambao wapo majumbani na wale ambao bado hawajaelewa au elimu haijawafikia ya kujikinga na ugonjwa huu wa Corona pamoja na wale ambao wamesikia lakini bado wanapuuzia .
Hata hivyo aliahidi kuendelea kusaidia zaidi katika maeneo mengine yenye mkusanyiko kuhakikisha wananchi wanadhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo.
No comments: