WANAFUNZI 1800 WA SHULE YA ST.JUDE ARUSHA KUNUFAIKA NA VIFURUSHI VYA MASOMO WAKIWA MAJUMBANI



Vero Ignatus,Arusha
 
Shule ya St Jude imebidi itumie ubunifu ili kuwasaidia wanafunzi kuendelea kujifunza na kuwa na motisha ya kusoma baada ya waalimu kutengeneza vifurushi vya kujisomea,ambavyo vina vitini vya kila somo, karatasi za kazi, na mitihani ya mock ya kufanyiwa nyumbani kwa wanafunzi wa madaraja yote

Shule hiyo yenye wanafunzi wanaotoka katika Kaya masikini ya St Jude iliyopo mkoani Arusha, imezindua mpango mpya wa kuendelea kuwafundisha wanafunzi wao bure wakiwa majumbani kwa kusambaza vifurushi vya masomo kwa kutumia mabasi 25.

Akizungumza na Michuzi Blog Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa shule ya St Jude Gemma Sisia alisema mpango huo mpya, unalenga kuwafikia wanafunzi 1800 wa shule hiyo,kwa Sababu wanafunzi wao wengi hawana uwezo kwa kuwa na vifaa vya teknohama vya kujifunza nyumbani.

"Shule imebidi itumie ubunifu ili wanafunzi waendelee kujifunza na kuwa na motisha ya kusoma baada ya Waalimu kutengeneza “vifurushi vya kujisomea”, ambavyo vina vitini vya kila somo, karatasi za kazi, na mitihani ya mock ya kufanyiwa nyumbani kwa wanafunzi wa madaraja yote"alisema Mkurugenzi Sisia

Mkurugenzi huyo alisema njia hiyo imeanza kuonesha mafanikio makubwa kwani wanafunzi wanapofikishiwa vifurushi huanza kujisomea na wana fursa kuwasiliana na walimu wao.

Sisia alisema usambazaji wa kivurushi hivi vya kujisomea kwa makazi ya kila mwanafunzi wao haujawa rahisi, shule imebidi itumie mabasi yao yote 25 kukamilisha kazi hiyo, pamoja na wazazi wawakilishi wa kila wilaya ili kusaidia kusambaza.

"Tunashukuru sana ushirikiano wa walimu, madereva wa mabasi na wazazi katika kusambaza vifurushi hivyo umekua wa kujivunia na wanafunzi wetu wote 1800 wamepata vifurushi"alisema

Aidha mkurugenzi huyo aliwataka wanafunzi na wazazi kuendelea kuchukuwa tahadhari kama ambazo shule hiy inafanya kwa waalimu wakati wa maandalizi ya vifurushi vya kujisomea,Kusafishwa kwa mabasi kwa vitakasa mikono kabla na baada ya kusambaza vifurushi hivyo.

No comments: