WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA WALEZEA ULIVYOJIPANGA KUKABILI MAJANGA YA MOTO KWENYE MISITU,MASHAMBA

 Moto ukiendelea kuwaka kabla ya kuanza kuzima na ntambo wa zima moto
 Mtambo wa zima moto ukirusha maji umbali wa mita 100 kuzima moto uliokuwa unawaka katika eno hilo wakati wa tukio la uzinduzi wa mtambo huo uliofanyika Mlandizi mkoani Pwani
 Mtambo wa kuzima moto ukiendelea kutoa maji kwa ajili ya kuzima moto uliokuwa umewashwa na watumishi wa TFS kwa ajili ya kuonesha uwezo wa mtambo huo kwenye kuzima moto
 Watumishi wa TFS ambao wamepata mafunzo ya kuzima moto kwa kutumia mtambo huo wakionesha ujuzi wa kuzima moto mbele ya Kamishna Muhifadhi wa TFS Profesa Dos Santos Silayo
 Kamishna Muhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania( TFS) Profesa Dos Santos Silayo akiwasha mtambo wa gari ya zima moto kama ishara ya kukabidhiwa rasmi mtambo huo leo
 Kamishna Mhifadhi wa TFS Profesa Dos Santos Silayo akitoa cheti kwa mmoja wa watumishi ambao wamepata mafunzo ya kutumia mtambo wa zima moto
 Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)wakiwa kwenye gari ya zima moto ambayo ni mali ya Wakala huo kwa ajili ya kukabiliana na majanga ya moto kwenye misitu asili na mashamba ya miti.Mtambo huoww kuzima moto umekabidhiwa leo kwa Kamishina Mhifadhi wa TFS Profesa Dos Santos Silayo( hayuko pichani)
Kamisha Mhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania( TFS) Profesa Dos Santos Silayo akizungumza leo akiwa Mlandizi mkoani Pwani baada ya kukabidhiwa ntambo wa zima moto kutoka kwa Kampuni ya Equator SumaJKT ambao ndio walioutengneza.
 Maji yakirushwa angani kutoka kwenye mtambo wa kuzima moto kama ishara ya uzinduzi rasmi wa kuanza kazi kwa mtambo huo ambao umekabidhiwa leo kwa TFS

 

Na Said Mwishehe,Michuzi TV

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)umesema katika kukabiliana na majanga ya moto kwenye mashamba ya miti na misitu asili watahakikisha wanunua mitambo ya kisasa na yenye uwezo mkubwa wa kuzima moto kwenye kanda zao zote saba ili kuhakikisha inakuwa salama wakati wote.

Umefafanua moja ya changamoto kubwa ambayo wanakumbana nayo ni misitu kuungua moto na kusababisha hasara kubwa ambapo kwa mwaka 2019 hasara  ambayo wameipata Ni kuungua miti yenye thamani ya Sh.bilioni tano tena kwenye Shamba moja la miti Sao Hili,hivyo kuwa na mitambo ya kuzima moto Ni moja ya kipaumbele chao.

Akizungumza leo Mei 4 mwaka 2020 Ruvu mkoani Pwani wakati wa kukabidhiwa mtambo wa kuzima moto ambao umetengenezwa na Kampuni ya Equator SumaJKT Ltd,Kamishna Mhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania( TFS) Profesa Dos Santos Silayo amesema mtambo ambao wamekabidhiwa ni maalum kwa kuzima moto katika mapori na misitu na ni wa kwanza hapa nchini.

"Kama mnavyofahamu sekta ya misitu ni muhimu sana katika ukuaji wa sekta nyingine na sisi kama Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania tunaowajibu wa kulinda misitu na mapori kutoka kwenye matishio yoyote. Na tishio mojawapo katika misitu yetu ni moto ambayo inaweza kuanza bila kuratibiwa na hatimaye kuangamiza misitu na kuharibu ikolojia nzima kwa hiyo ni wajibu wa Serikali kuhakikisha uwekezaji unaofanywa katika misitu unakuwa salama,"amesema

Amesema kuwa mashamba ya miti wanayopanda na hifadhi za Misitu asili nayo inakuwa salama , hivyo waliona haja ya kuzungumza na  SumaJKT kwa ajili ya kutengeneza mtambo huo ambao umegharimu zaidi ya  Sh.milioni 700 .

"Jukumu letu la kwanza TFS ni kuhakikisha moto hauanzi lakini hata unapokuwa umeanza lazima wapambane nao na hivyo vifaa ni muhimu kwa mtambo ambao tumekabidhiwa leo unauwezo mkubwa ukiwemo wa kuzima moto umbali wa mita 100 tofauti na mitambo mingine iliyopo nchini.Mtambo huu utakwenda kuhudumia misitu lakini pia utatoa fursa ya kusaidia maeneo yanayozunguka misitu pamoja na mali za wananchi.

"Tunaamini wenzao wa Suma JKT wataongeza ubunifu wakati na sisi tukiendelea kununua mitambo mingine kwa ajili ya kuitawanya katika misitu kwa ajili ya kukabiliana na majanga ya moto yanayoweza kujitokeza. Watalaam ambao wamefundishwa kuutumia mtambo huo ujuzi wao utakwenda kuongeza tija ya kukabiliana na moto," amesema Profesa Silayo.

Kuhusu mipango ya baadae,  amesema ni kuwa na mitambo ya kuzima moto kwenye kanda zote saba kwa kuhakikisha kila Kanda inakuwa na mtambo wake wa kuzima moto huku akielezea umuhimu wa kuelimisha umma kutunza misitu.

"Kwa bahati mbaya matukio ya moto yamekuwa yakitupata na kusababisha  hasara kubwa, mwaka jana tumepata hasara ya Sh.bilioni tano kutokana na miti kuungua.Na miti iliyoungua ilikuwepo ya kuanzia mwaka mmoja mpaka miaka 17, hivyo unapata hasara ya miti iliyotegemea kuvuna miaka 20 ijayo.

"Kwa hiyo kama huna uwezo wa kupambana na moto maana yake utakuwa unapanda miti kila baada ya muda fulani kwasababu tu inaungua moto. Hivyo unapokuwa na mitambo ya kuzimia moto maana yake unakuwa na uwezo wa kulinda miti ambayo mwisho wa siku inavunwa na kuingiza kwenye biashara ili Serikali ipate fedha,"amesema Profesa Silayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Equator SumaJKT Ltd  Robert Mangazeni amesema mtambo huo ambao wameukabidhi leo unaouwezo mkubwa na kwa jinsi ambavyo umetengenezwa unaouwezo wa kuhimili mazingira ya aina yoyote na kwamba gharama ya fedha iliyotumika kuitengeneza Ni Sh.milioni 700 wakati huko nyuma kuna mitambo ilinunuliwa kutoka nje ya nchi iligharimu zaidi ya Sh.bilioni 1.2 kwa mtambo mmoja.

Hivyo amesema wao kupitia Kampuni hiyo wametengeneza mtambo mkubwa na wa.kisasa kwa gharama za chini kabisa na inaweza kutumika kwenye Misitu, majiji na viwanja vya Ndege na kuongeza ni mtambo ambao kwa Tanzania na nchi za Afrika ni wa kwanza.

Wakati huo huo Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi wa Misitu Shamba la Miti Sao Hili Salum Yakut ambaye Ni moja ya watumishi wa TFS waliofundishwa kutumia mtambo huo amesema unakwenda kuongeza ulinzi wa miti ndani ya shamba hilo.

No comments: