UVIKASA YAKABIDHI PIKIPIKI 32 NA VIFAA KINGA KWA VIJANA.
Na Abdullatif Yunus Michuzi TV.
Uongozi wa Umoja wa Vijana Karagwe Saccos (UVIKASA) kupitia Mlezi wake Mbunge wa Karagwe na Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent L. Bashungwa umekabidhi pikipiki 32, pamoja na Vifaa kinga dhidi ya Corona kwa vijana wanachama wa Saccos hiyo ili kuwaendeleza kiuchumi.
Tukio hilo limefanywa na Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti mapema Mei 07, 2020 katika Viwanja vya Ofisi za CCM Karagwe, na kushuhudiwa na Viongozi wa Chama na Serikali, ikiwa ni Sehemu ya kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli kuwainua Vijana kiuchumi na huo ukiwa ni muendelezo wa Saccos hiyo kutoa mikopo na fedha kwa Vijana Wanachama wake.
Akitaja Vifaa vilivyokahidhiwa kwa Vijana hao Mwenyekiti Mwanzilishi wa Saccos hiyo Ndg. Yahya Kateme ametaja kuwa ni pamoja na pikipiki 32 zenye thamani zaidi ya shilingi Milioni 72, Vitaka mikono (sanitizer) na Barakoa zenye thamani zaidi ya shilingi Milioni Mbili, lengo likiwa ni kuendelea kupambana na janga la Corona, kwa kujilinda na kuwalinda wengine, huku akiongeza kuwa mpaka sasa tayari pikipiki 1050 zenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.7 zimekwisha tolewa.
Aidha katika Shukrani zake Mweyekiti Yahya amemshukuru Mkuu wa Mkoa pamoja na Vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwemo TAKUKURU kwa namna ambavyo wamesaidia kurejeshwa kwa mikopo iliyokuwa nje kwa wadaiwa sugu, hali iliyopelekea kuiinua tena Saccos hiyo iliyoonekana kuanza kuchechemea.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vitendea kazi hivyo Mkuu wa Mkoa Kagera Brig. Jenerali Marco Gaguti amewataka Vijana hao kutunza na kuvitumia kwa umakini, ili viweze kuwainua kama ilivyokusudiwa na kuongeza kuwa huo ni mwendelezo wa Taasisi hiyo ya fedha, baada ya jitihada za muda mrefu.

Pichani ni moja kati ya Vijana 32 akionesha Namba ya Usajili ya Pikipiki yake mara baada ya kukabidhiwa chombo hicho na Mkuu wa Mkoa wa Kagera katika Viwanja vya CCM Wilayani Karagwe.
Pichani Mkuu wa Mkoa wa Kagera akikabidhi Pikipiki mojawapo kati ya Pikipiki 32 zilizotolewa kwa UVIKASA kupitia fedha za marejesho, pipikpi hizo ni mkopo kwa Vijana kuwainua kiuchumi.
Pichani ni moja kati ya Vijana 32 akionesha Namba ya Usajili ya Pikipiki yake mara baada ya kukabidhiwa chombo hicho na Mkuu wa Mkoa wa Kagera katika Viwanja vya CCM Wilayani Karagwe.
Pichani ni baadhi ya Pikipiki 32 zilizotolewa kwa Vijana wa Wilaya za Karagwe na Kyerwa zenye thamani jumla ya Shilingi Milioni 72 ikiwa ni mwendelezo wa mkopo Kwa Vijana hao kuwainua kiuchumi.
Pichani Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe. Gaguti akikagua moja kati ya Barakoa 2000 zilizotolewa pamoja na vitakasa Mikono kwa Bodaboda na Vijana waliopata mkopo wa Pikpipiki Wilaya za Karagwe na Kyerwa.
No comments: