SIRI YA VIJORA VYA MAMA CHOGO
MSANII anayekimbiza kwenye tasnia ya uchekeshaji nchini, Abdallah Sultan a.k.a Dulvan amezindua rasmi shindano la "Asante fans".
Dullvan amesema kuwa kutokana na kupokelewa kwake vizuri na mashabiki zake ameamua kurudisha fadhila kwa mashabiki zake kupitia shindano hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa vigezo vya kushiriki kwenye shindano hilo ni kumfwatilia kwenye mitandao yake ya kijamii kwa njia ya kuchangia ujumbe mfupi na kuwatag watu wa tano kwenye picha ambazo atakuwa anatuma kwenye mtandao wake wa Instagram na kupata mshindi.
"Shindano hilo litakuwa kwa kila wiki kwa njia ya simu na hii nimeamuwa kufanya hivyo kwa lengo la kurudisha asante kwa mashabiki zangu kwa mafanikio ambayo nimepata tangu nimeanza kazi zangu za uchekeshaji"
Aliongezea kuwa kwa wikii hii mshindi atapata kiasi cha fedha laki 5 kwa watu wa tano na shindano alichagui ni kwa watu wote.
Hata hivyo dullivan ameeleza kuwa jamii inayomzunguka bado inaendelea kumpa nguvu hasa mama yake mzazi tangu ameanza kazi hiyo mpaka Sasa hivyo hategemei kukatishwa tamaa kutokana na kuvaa uhusika wa kike (mama chogo) kuanzia mavazi,lafudhi pamoja na madoido .
''wakati mwingine mama yangu mzazi mwenyewe ananichagulia mavazi Kama vijora na ananishauri kabisa vitanipendeza kutokana na rangi zake hivyo naona ndio baraka ananimwagia na anachukulia Kama kazi zingine tu ndio maana nafanikiwa napata kazi nyingi na ndio maana napata na mimi nguvu ya kurudisha fadhila kwa mashabiki,".
No comments: