SERIKALI YAWAKATA WAKULIMA SHINYAGA KUCHANGAMKIA FURSA ZA VIWANDA
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe katikati akiangalia mashine ya kuoka mikate iliyobuniwa na Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) Tawi la Shinyanga kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Bw.Ludovick Nduhiye na Kushoto kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Albert Msovela.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe amoja na Mkurugenzi wa kiwanda kinachozalisha mafuta ya alizeti Gilitu Enterprises Bw. Gilitunila Makula wa pili kushoto, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Bw.Ludovick Nduhiye wa pili kulia walipofika kiwandani hapo kujionea namna kinavyozalisha mafuta ya Alizeti.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa kiwanda kinachozalisha mafuta ya alizeti Gilitu Enterprises Bw. Gilitunila Makula wa pili kushoto pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Bw.Ludovick Nduhiye.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Albert Msovela akifafanua jambo kuhusu Mashine ya kuoka mkate iliyobuniwa na SIDO Shinyanga kwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe aliyongozana na Naibu Katibu Mkuu wake Bw.Ludovick Nduhiye.
****************************
Na mwandishi wetu Shinyanga
Serikali imewataka wakulima mkoani Shinyanga kutumia mbegu bora za pamba pamoja na Alizeti ili kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mafuta yatokanayo na mazao hayo ili viwanda vya usindikaji mafuta viweze kuzalisha mafuta kwa wingi na yenye ubora kukidhi viwango vya kimataifa.
Akiongea wakati wa ziara ya Siku moja katika Manispaa ya Shinyanga Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe amesema uwepo wa Viwanda vya kusindika mafuta pamoja na nyama Mkoani Shinyanga ni fursa kwa wakazi na wakulima wa Mkoa huo kuzalisha mazao ya Alizeti na pamba kwa wingi kwani Viwanda hivyo vinauza mafuta yake ndani na nchi.
Aidha Prof. Shemdoe ameagiza uongozi wa kiwanda cha kutengeneza nyuzi kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya Shinyanga kubadili mkakati wa biashara na kuanza kuuza malifghafi hiyo katika Viwanda vya ndani tofauti na sasa ambapo malighafi hiyo inauzwa kwa wingi Nchini China.
Kiwanda hicho kwa sasa kimesitisha uzalishaji kwa muda kutokona na changamoto ya ugonjwa wa Covid 19 kwa kuwa baadhi ya wataalam wa kiwanda hicho wamekwama Nchini China na hali ikiwa shwari watarejea Nchini kwa ajili ya uzalishaji kiwandani hapo.
‘’Vipo Viwanda vya nguo hapa Nchini ambavyo vingefaidika na malighafi ya kiwanda hiki lakini kwa kuwa utaratibu wa kiwanda hiki wa kuuza nje nyuzi kwa 80% na kubakiza 20% hapa Nchini una athari kwa Viwanda ndani kaeni na EPZA ili kubadili sheria ili nyuzi zinazolishwa hapa Nchini zieweze kunufaiusha Viwanda vya ndani.” Aliendelea kusema Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe.
Prof. Shemdoe amesema kuwa Serikali kwa sasa ina jumla ya Viwanda 8477 kote Nchini ambavyo vimejengwa kwa kipindi cha serikali ya awamu ya tano jambo linaloifanya Tanzania kuendelea kuwa Serikali ya Viwanda jambo ambalo litatoa fursa za ajira kwa wananchi wengi Zaidi hapa Nchini.
Kiongozi huyo wa Wizara pia alikagua na kutembelea kiwanda cha uchakataji nyama ya Punda ambacho na kuwataka wazalishaji wa nyama hiyo kuzingatia masharti ya Kibali cha Wizara ya Mifugo waliyopewa ya kuchinja Punda 30 kwa siku ikiwemo na kuleta mbegu ya kunenepesha Punda wa hapa Nchini kwa lengo la kuongeza uzalishaji.
‘’Nimeuliza wenzangu wote hapa hakuna mtumiaji wa Nyama hii ambayo inauzwa nje ya Nchi hivyo wazalishaji wanyama hii wanasafirisha nyama hii Nchini china kwa 100% na wako ndani ya eneo la EPZA hivyo wananchi watumie fursa hii kufuga Punda kwa wingi ili waweze kunufaika na uwepo wa kiwanda hiki’’.Alisisitiza Prof. Shemdoe.
Katibu Mkuu Shemdoe yupo Mkoani Shinyanga kutembelea maeneo ya uwekezaji yaliyoko Mkoani humo ziara ambayo imekuwa ikiendelea kwa Wilaya za Kahama na Manispaa ya Shinyanga ambapo amejionea maeneo ya uwekezaji pamoja na Viwanda vilivyopo Shinyanga.
No comments: