RC TANGA AWATAKA WANANCHI TANGA KUACHA HOFU,BADALA YAKE WAENDELEE KUCHUKUA HATUA YA KUJIKINGA NA CORONA
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela akiwa katika moja ya vikao vyake vya mara kwa mara vinavohusiana na mapambano dhidi ya Corona, Pichani akiwaonesha Wajumbe Vazi Maalumu la Wataalamu wanaohudumia wagonjwa wa COVID-19 Mkoani Tanga.
Aidha amesema kuwa serikali imeendelea kujidhatiti na kufanya kazi kwa ushirikiano katika kipindi hiki pia kuhakikisha inawajali sana na kuwapa kipaumbele wataalamu wa Afya.
Zaidi amewaomba wana Tanga kuacha hofu kama anavyosisitiza Raisi wetu wa Dk.John Pombe Magufuli zaidi kuendelea kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalam wetu wa Afya na kuhakikisha tunakua salama huku kwa tahadhari kubwa na umakini sana tukiendelea kufanya kazi.
No comments: