RAIS DK. MAGUFULI AFIKIRIA KURUHUSU LIGI KUU TANZANIA BARA KUENDELEA

Na Said Mwishehe, Michuzi TV.

BAADA ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara pamoja na aina nyingine za ligi za michezo mbalimbali kusimama kutokana na janga la Corona, Rais Dk.John Magufuli amesema anaangalia uwezekao wa kuruhusu ligi kuendelea ili Watanzania wawe wanaangalia ligi hizo.

Ametoa kauli hiyo leo akiwa Chato mkoani Geita baada ya kumuapisha Waziri mpya wa Katiba na Sheria Dk.Mwigulu Nchemba ambapo Rais amefafanua anafikiria kwa siku zinazikuja aruhusu ligi iendelee angalau watu wawe wanaangalia luninga.

"Kwasababu naelewa hata kwenye eneo la michezo sijaona mwanamichezo yoyote ambaye amedhurika sana na Corona.Hii inadhihirisha kwa wale wanaofanya mazoezi Corona inawakwepa,sasa kama tunawazuia kucheza hata mpira maana yake tunawaambia waugue Corona.

"Itafika mahali hata ligi tuendelee kucheza, inaweza kuishi na huu ugonjwa kama wanavyoishi watu wenye Ukimwi,TB na Surua.Tuache uoga, tuache kutishana,"amesema Rais Magufuli.
 

No comments: