Profesa Mdoe akagua ukarabati, ujenzi wa chuo kikuu Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe akisaini kitabu cha wageni mara bada ya kuwasiri katika chuo kikuu cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam-Tegeta, kwaajili ya kuangalia maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa Vyumba vya madarasa.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe akiwa ameamatana na wafanyakazi wa chuo kikuu cha mzumbe  wakitembelea majengo ya  chuo kikuu cha Mzumbe jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe akikagua miundombinu na madarasa katika chuo kikuu cha Mzumbe  Dar es Salaam-Tegeta.
 Naibu makamu mkuu, utawa na fedha wa chuo kikuu cha mzumbe Profesa Ernest Kihanga akitoa maelekezo kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi na ujenzi wa chuo Kikuu cha Mzumbe jijini Dar es Salaam.
 Muonekano wa Maktaba katika chuo hicho.
Mkuu wa Chuo Kampasi ya Dar es Salaam, Honest Ngowi akionesha mipaka ya chuo kikuu cha Mzumbe jijini Dar es Salaam, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi na ukarabati wa vyumba vya madarasa katika chuo hicho.
Muonekano wa baadhi ya majengo katika chuo kikuu kampasi ya Tegeta jijini Dar es Salam.

NAIBU Katibu Mkuu  Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe amehitimisha ziara yake Chuo Kikuu Mzumbe kwa kutembelea na kukagua ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya kampasi ya Dar-es-salaam Tegeta ambacho kimekusudiwa kuanza kutoa  Shahada za Awali Kwa mwaka 2020/2021.

Aidha, amepongeza hatua kubwa iliyofikiwa hadi sasa katika ujenzi wa nyumba za madarasa na mihadhara na   kupendekeza ujenzi unaoendelea kuendana na mahitaji ya sasa ya mabadiliko ya teknolojia, kwa kuwezesha matumizi ya teknolojia katika ufundishaji.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Naibu Makamu Mkuu chuo Prof Ernest Kihanga amesema ukarabati huo ulianza Juni 2018 ukiwa ni upanuzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam na kwamba ujenzi umekamilika kwa asilimia 99, na majengo yako tayari kuanza  kutumika pindi idhini ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) itakapotolewa.

Amesema chuo hicho kitakuwa na Maktaba, ofisi za walimu, vyumba vya madarasa na mihadhara, chumba cha komputa na huduma nyinginezo muhimu kumwezesha mwanafunzi kusoma. 

Kuanzishwa kwa programu za Shahada za awali kwa Kampasi ya Dar-es-Salaam kutaongeza wigo wa vijana wengi zaidi kujiunga na elimu ya juu nchini sambamba  na kuongeza fursa za ajira.

No comments: