MASHAIDI 19 KUTOA USHAIDI KESI YA DAWA ZA KULEVYA
MAHAKAMA Kuu kitengo cha Uhujumu Uchumi jijini Dar es Salaam imeelezwa kuwa jumla ha mashahidi 19 wanatarajiwa kutoa ushahidi wao katika kesi ya kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya inayomkabili Gudluck Mbowe na Ally Mtema
Wakili wa serikali Costantine Kakula amedai hayo leo Mei 22, 2020 mbele ya Jaji Immaculata Banzi wakati akiwasomea hoja za awali washtakiwa hao.
Pia wakili Kakula amedai pamoja na mashahidi hao, upande wa mashtaka utawasilisha vielelezo mbalimbali ikiwemo mabegi saba ya bangi na gari aina yĆ Toyota Ist.
Akisoma hoja hizo za awali, Kakula amedai washtakiwa walikamatwa Oktoba 15 mwaka 2017 eneo la Kibaha kwa Matiasi baada ya polisi kupewa taarifa kwamba watu hao wamebeba dawa za kulevya katika mabegi saba ya bangi katika gari lao aina ya Toyota Ist.
Imeelezwa kuwa, siku ya tukio ,polisi eneo la Kibamba walijaribu kusimamisha gari hilo lakini hawakusimama na dereva aliendelea kundesha kwa mwendo kasi kitendo kilichopelekea polisi kulikimbiza gari hilo hadi lilipoingia mtaroni na kupata ajali, washtakiwa walikamatwa na ndipo upekuzi ulipofanyika.
Amedai, upekuzi huo ulihusisha washtakiwa pamoja na shahidi wa Kujitegemea na kufanikiwa kukamatwa kwa mabegi saba ya Bangi.
Hati ya upekuzi ilijazwa na kusainiwa na washtakiwa pamoja na shahidi huyo. Katika mahojiano washtakiwa hao wakiliri kubeba dawa hizo za kuevya.
Aidha imedaiwa kuwa, ripoti ya mkemia mkuu wa serikali ilithibitisha kwamba mzigo huo ni dawa za kulevya aina ya bangi kilo 128.54.
No comments: