MAMBO YA NDANI YAENDELEA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA UGONJWA WA COVID-19


Mkurugenzi Msaidizi Rasilimaliwatu, Hilda Tegwa (Wa tatu kulia) akisisitiza matumizi ya kunawa mikono kwa baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ili kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Covid-19. Tukio hilo limefanyika leo katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Rasilimaliwatu, Hilda Tegwa (Wa tatu kulia) akitakasa mikono yake kwa ajili ya kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Covid-19, wengine ni baadhi ya Watumishi wa  Wizara hiyo wakisubiri kutakasa mikono yao kabla ya kuingia katika Ofisi za Wizara hiyo, Jijini Dodoma leo.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya kuzuia na kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakitazama moja kati ya vifaa kwa ajili ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 kwa Watumishi wa Wizara hiyo na wageni wanaofika katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya kuzuia na kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakitazama moja kati ya vifaa kwa ajili ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 kwa Watumishi wa Wizara hiyo na wageni wanaofika katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakitakasa mikono yao katika moja ya kifaa kwa ajili ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 kwa Watumishi wa Wizara hiyo na wageni wanaofika katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma

No comments: