Kitengo cha uhandisi Mitambo kuhakikisha viwango vya bidhaa zinazalishwa ndani na nje ya nchi

*TBS iko kwa ajili ya kuweka Viwango vya Kitaifa.
*Miradi ya Ujenzi mbalimbali wa Serikali unatumia bidhaa za Viwanda vya ndani kutokana Viwango kufikiwa

Na Ripota wetu-Michuzi TV.

Kitengo Cha Uhandisi wa Mitambo wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kimesema kuwa Nondo, Bati na Misumari na bidhaa zingine za kiuhandisi zimekuwa na viwango na kukubalika katika Kanda mbalimbali

Akizungumza na michuzi Tv Afisa Viwango Mwandamizi Kitengo Cha Uhandisi Mitambo wa TBS Joseph Mwaipaja amesema kuwa tangu kuanizishwa kwa Kitengo hicho wameshapima Viwango bidhaa 400.

Amesema Viwanda vya ndani vinazalisha bidhaa za kiuhandisi kwa Viwango na kufanya miradi Ujenzi inayoendelea wanatumia bidhaa hizo ikiwa ni pamoja na kulinda Viwanda hivyo viendelee kuzalisha bidhaa hizo.

Mwaipaja amesema  kuwa changamoto zilizopo kwa baadhi ya wafanyabiashara kuingiza bidhaa ambazo hazina Viwango vilivyowekwa na Taifa katika bidhaa husika.

Amesema wakati wa kutaka kuagiza bidhaa za bomba, mita za maji kuwasiliana na TBS Kuweza kupata Viwango halisi ili kuepuka hasara wakati wa mzigo unafika nchini.

Aidha amesema kuwa Viwango vinavyowekwa Ni vya Taifa na sio Viwango vya TBS kwa watu wapo kwa ajili ya kusaidia wananchi.

Hata hivyo amesema TBS itahakikisha wananchi wote wanapata huduma za bidhaa za kiuhandisi zenye Viwango.

Bidhaa za Kiuhandisi ni mabomba ya plastiki, mabomba ya Chuma, Misumari,Bati, pamoja na Nondo.
 Afisa Viwango Mwandamizi Kitengo Cha Uhandisi Mitambo  wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Joseph Mwaipaja akizungumza na Michuzi TV kuhusiana na Viwango katika bidhaa za kiuhandisi ikiwemo Nondo,Bati ,Misumari pamoja mabomba ya palatiki na Chuma.
 Afisa Viwango Mwandamizi Kitengo Cha Uhandisi Mitambo  wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Joseph Mwaipaja akizungumza na Michuzi TV kuhusiana na Viwango katika bidhaa za kiuhandisi ikiwemo Nondo,Bati ,Misumari pamoja mabomba ya palatiki na Chuma.

No comments: