Kitengo cha uhandisi Mitambo (TBS) kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa ndani na nje ya nchi zinakidhi kiwango husika

Afisa Viwango Mwandamizi Kitengo Cha Uhandisi Mitambo wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Joseph Mwaipaja akizungumza na Michuzi TV kuhusiana na Viwango katika bidhaa za kiuhandisi ikiwemo Nondo,Bati ,Misumari pamoja mabomba ya palatiki na Chuma.
Afisa Viwango Mwandamizi Kitengo Cha Uhandisi Mitambo wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Joseph Mwaipaja akizungumza na Michuzi TV kuhusiana na Viwango katika bidhaa za kiuhandisi ikiwemo Nondo,Bati ,Misumari pamoja mabomba ya palatiki na Chuma.

*TBS iko kwa ajili ya kuweka Viwango vya Kitaifa.
*Miradi ya Ujenzi mbalimbali ya Serikali inatumia bidhaa za Viwanda vya ndani kutokana Viwango kufikiwa.

Na Mwandishi Wetu.
KITENGO Cha Uhandisi wa Mitambo cha Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kimesema kuwa Nondo, Bati na Misumari na bidhaa zingine za kiuhandisi zimekuwa na viwango na kukubalika katika masoko ya Kanda mbalimbali

Akizungumza na michuzi Tv Afisa Viwango Mwandamizi Kitengo Cha Uhandisi Mitambo (TBS) Joseph Mwaipaja amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa Kitengo hicho wameshaandaa Viwango zaidi ya 400.

Amesema Viwanda vya ndani vinazalisha bidhaa za kiuhandisi zilizokidhi Viwango na kufanya miradi ya Ujenzi inayoendelea kutumia bidhaa hizo ikiwa ni pamoja na kulinda Viwanda hivyo viendelee kuzalisha bidhaa hizo na kupata soko kiurahisi ndani na nje ya Tanzania.

Mwaipaja amesema kuwa changamoto zilizopo kwa baadhi ya wafanyabiashara ni kuingiza bidhaa ambazo hazina ubora kwa kutokukidhi viwango vya bidhaa husika vilivyowekwa na Taifa kupitia TBS.

Amesema wakati wa kutaka kuagiza bidhaa za bomba, mita za maji ni vyema kwa waagizaji kuwasiliana na TBS ili Kuweza kupata Viwango halisi ili kuepuka hasara ya kumlazimu kuurudisha au kuuteketeza pale mzigo unapofika nchini chini ukiwa chini ya kiwango.

Aidha amesema kuwa Viwango vinavyowekwa Ni vya Taifa na sio Viwango vya TBS, TBS wapo kuratibu uandaaji wa viwango hivyo kwa ajili ya kusaidia wafanyabishara kufanya biashara bila vikwazo na kuhakisha wananchi wanapata kilicho bora na salama.

Hata hivyo amesema TBS itahakikisha wananchi wote wanapata huduma za bidhaa za kiuhandisi zenye Viwango.

Bidhaa za Kiuhandisi ni mabomba ya plastiki, mabomba ya Chuma, Misumari,Bati, pamoja na Nondo.

No comments: