KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AKUTANA NA MAAFISA WAANDAMIZI WA MAGEREZA WALIOHAMISHIWA MAKAO MAKUU YA JESHI HILO DODOMA HIVI KARIBUNI



Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee akizungumza katika kikao kazi na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza ambao wamehamishiwa hivi karibuni Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, jijini Dodoma. Kikao hicho kimefanyika leo Mei 19, 2020 kwa lengo la kupeana mikakati mbalimbali ya kazi sambamba na maelekezo ya utekelezaji wa mageuzi yanaendelea ndani ya Jeshi hilo.
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini maelekezo kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee(hayupo pichani)katika kikao kazi kilichofanyika leo Mei 19, 2020 Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dodoma.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee(meza kuu) akiwa na Kamishna wa Utawala na Rasilimali watu wa Jeshi la Magereza, Uwesu Ngarama(kulia) pamoja na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Magereza, SACP. Mzee Nyamka(kushoto) wakifuatilia kikao kazi cha MaafisaWaandamizi wa Jeshi hilo kilichofanyika leo Mei 19, 2020, Jijini Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu katika Jeshi la Magereza, SACP. Boyd Mwambingu akiteta jambo na Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee mara baada ya kikao kazi na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza ambao wamehamishiwa hivi karibuni Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, jijini Dodoma(Picha zote na Jeshi la Magereza).

No comments: