KAMALA AWASHAURI VIJANA WENZAKE KUTOTUMIA VIBAYA MITANDAO HIYO YA KIJAMII.

Na, Irene Mwidima, Globu ya jamii.

John George Kamala, Kijana anayejihusisha na masuala ya mitindo (model) amewataka vijana kutokutumia vibaya mitandao ya kijamii bali waitumie kujiingizia kipato.

Kamala pia amekuwa moja ya vijana wanaojiingizia kipato kupitia mtandao wa kijamii YouTube.

Amesema, ukiitumia vizuri mitandao ya Kijamii inakuleta manufaa makubwa sana bila kumtegemea mtu akusaidie na zaidi utajulikana kwa upana zaidi na watu mbalimbali.

Kamala amewasihi vijana wote kuacha kutumia vibaya mitandao ya kijamii na kutaka kuitumia kwa manufaa haswa kwa kipindi hiki cha janga la corona kama kusambaza taarifa zisizo sahihi na za uongo zinazo zushwa mitandaoni.

“Vijana wengi wamekuwa wakisambaza picha ambazo sio za desturi yetu watanzania ili kuharibu au kuchafua sifa ya mtu fulani kwa mapendo au kwa ajili ya lengo fulani ambapo tatizo hilo linakuwa sio maadili mazuri kwetu sisi.” amezungumza hayo Kamala.

Aidha amesema “Sisi tunanguvu kubwa sanaa katika taifa letu lakini wengi wetu hukata tamaa mapema sana, tuna vivutio vingi sana nchini tunatakiwa kutumia hivyo vivutio vyetu kuitangaza nchi yetu kwa upana zaidi ili kuruhusu utalii kwa kiwango kikubwa katika nchi yetu’’

Kamala amesema ya kwamba yeye binafsi anaiongoza na kuiendesha kurasa yake ya YouTube ifahamikayo kama Camalavlogs haswa katika mambo yake yote ya siku na kutangaza kazi zake akishirikia na watu wa mataifa mengine na kuwafundisha utamaduni wetu wa asili ya Tanzania.

No comments: