CCM wamnasa Kigogo aliyewahi kuwa mkuu wa Idara ya Sera na Itifaki CHADEMA

Na Amiri Kilagalila,Njombe

Aliyewahi kuwa katibu mkuu wa Chama cha NCCR Mageuzi,Mkuu wa Idara ya Sera na Itifaki CHADEMA,Mjumbe wa kamati ya Ukawa na kampeni meneja wa Mgombea wa Makam wa Rais Ukawa Bwana,Juju Martin Danda amepokelewa na Chama cha Mapinduzi CCM na kukabidhiwa kadi ya Chama hicho na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe.

Akizungumza dhamira ya kujiunga na Chama hicho,Martin Danda amesema ni kutokana na uozo uliopo katika vyama vya upinzani.

“Nilifanya harakati nyingi sana katika kuvijenga vyama vya upinzani kwa maumivu makubwa na umaskini mkubwa sana,tumeijenga Chadema tumeipeleka kwenye vyuo vikuu,lakini kinachoendelea ndani ya vyama hivi ni uozo wa hali ya juu ambao wengine tulishindwa kuvumilia”alisema Danda

Vile vile amesema Vyama vya upinzani vimekuwa vinatengeneza wanaharakati wasiokuwa na ajenda wanao shinda kutukana.

“Kuna biashara ni vyama vinavyotengeneza wwanaharakati wasio kuwa na ajenda wanao shinda kutukana,lakini ukizungumza chama cha kujifunza katika bara la Afrika,namba moja ni Chama cha Mpainduzi”alisema tena Danda

Aidha ametaka watanzania kuendelea kuunga mkono kazi zinazofanywa na Rais Magufuli kwa kuwa amefanya kazi kubwa kwa kuendesha miradi mikubwa huku akipongeza namna hatua alizozichukuwa katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona na kuishangaza Dunia.

Naye katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe Erasto Ngole amesema kiongozi huyo sio mwanasiasa wa kawaida kutokana na uvumilivu aliokuwa nao zaidi ya Chaguzi tano akiwa Upinzani.

“Juju Danda tumekwaluzana zaidi ya chaguzi tano yuko upinzani,na huku Njombe akiwa na NCCR Mageuzi alikuwa na vijiji vichache na Vitongoji yote ilikuwa kazi ya huyu bwana kwa hiyo ndani ya CCM naamini tumempata mtu mzuri,kwasababu ndiye aliyepandikiza upinzani Njombe Kusini”alisema Erasto Ngole

Akizungumza baada ya kumpokea na kumkabidhi kadi mwanachama huyo Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Jassel Mwamwala,amesema wanakila sababu ya kuwapokea wanaorudi katika Chama hicho kutokana na Nguvu waliyonayo iliyotengenezwaq na serikali ya awamu ya Tano.

“Kwa heshima ya viongozi wangu wa Taifa na kwa niaba ya wanachama wa mkoa wa Njombe,nimempokea ndugu yetu Danda,na chama Cha Mapinduzi hakina Ubaguzi,hakina Dini wala kabila wote tunaheshimiana kama ambavyo katiba inasema”alisema Mwamwala

“Mwenzetu hapa amesema vizuri kuwa amefanya kazi kubwa sana,amesema amefanya kazi kwenye Ukawa,ameona kule hakuna amani,kuna uozo ndio maana amekuja kupata haki ya uanachama kutoa mawazo yake”aliongeza Mwamwala.
 Juju Martin Danda akiapishwa na katibu wa UWT Mkoa wa Njombe Marry Mkoka mara baada ya kukabidhiwa kadi ya Chama cha Mapinduzi.
 Juju Martin Danda Akikabidhiwa kadi ya CCM na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Jassel Mwamwala
 Aliyewahi kuwa katibu mkuu wa Chama cha NCCR Mageuzi,Mkuu wa Idara ya Sera na Itifaki CHADEMA,Mjumbe wa kamati ya Ukawa na kampeni meneja wa Mgombea wa Makam wa Rais Ukawa Bwana,Juju Martin Danda akizungumza sababu ya kuhamia Chama cha Mapinduzi

 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Jassel Mwamwala akizungumzia umahili wa kiongozi huyo alipokuwa upinzani.
 Katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe Erasto Ngole akieleza jinsi bwana Danda alivyoufikisha upinzani mkoani Njombe.
Baadhi ya viongozi wakati wa kumpokea aliyewahi kuwa kiongozi wa vyama vya upinzani.

No comments: