BANDARI KAVU KWALA MBIONI KUKAMILIKA ,NDITIYE AAGIZA USIMAMIZI KAMILIFU


NA MWAMVUA MWINYI,PWANI .

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye amesema ,ujenzi wa mradi wa bandari kavu Kwala,Kibaha mkoani Pwani ni utekelezaji wa maagizo ya Rais dkt.John Magufuli ya kupunguza msongamano kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

Kutokana na hilo ,Nditiye ameitaka Bodi ya Bandari kusimamia kikamilifu na kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa asilimia 100 ifikapo mwezi Juni 2020. Aliyasema hayo ,wakati wa mapokezi ya Treni ya kwanza iliyoleta makasha 20 kwenye Bandari Kavu ya Kwala iliyopo Ruvu Kibaha.


Aidha Nditiye ,alikubali ombi la mkoa wa Pwani la kuwepo kwa kituo cha Polisi kwenye eneo hilo ili kuimarisha ulinzi na Usalama hivyo amewataka TPA kuhakisha kunajengwa kituo hicho cha polisi.
Nae mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo anasema huo umejipanga kikamilifu kutumia fursa za kiuchumi na kijamii zinazotokana na Bandari hiyo. 

Alibainisha kuwa mkoa kupitia Halmashauri ya Wilaya Kibaha upo katika mchakato wa kuupanga Mji wa Kwala kuwa Mamlaka ya Mji Mdogo ili kuendana sambamba na ukuaji wa shughuli za kiuchumi kwenye eneo hilo. 

Ndikilo aliongeza kuwa mkoa umeanisha Ekari 4,000 ambazo zinazunguka Bandari kavu ya Kwala na Mji wa Kwala, Ekari hizo zitandaliwa Mpango wa Matumizi mbalimbali ambapo mchakato wa kukamilisha matumizi hayo unasimamiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi . Katika hatua nyingine Ndikilo aliwakaribisha wawekezaji wa viwanda kwenda Kwala kuchangamkia fursa zilizopo katika eneo hilo. 

Alisema eneo hilo lipo karibu na Bandari kavu Kwala, lipo karibu na SGR, lipo karibu na Reli ya TAZARA, lipo karibu na chanzo cha Maji DAWASA.”Wananchi wa Pwani na Wawekezaji tutumie fursa za Kiuchumi na Kijamii zinazotokana na Bandari hii” 
 

No comments: