WATEJA SOKO LA KIHESA WADAIWA KUKAIDI AGIZO LA KUTAKASA MIKONO
KaimuMeya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Joseph Ryata akiwa katika soko la Mlandege alipofanya Ziara katikamasoko ya manispaa ya Iringa kwa lengo la kujua namna gani wafanyabishawanaelimu ya kupambana na Virusi vya Corona
KaimuMeya wa Halmashauri ya Manispaa yaIringa Joseph Ryata akiwa katika soko la Ipogolo alipofanya Ziara katikamasoko ya manispaa ya Iringa kwa lengo la kujua namna gani wafanyabishawanaelimu ya kupambana na Virusi vya Corona
Kaimu Meya wa Halmashauri ya Manispaa yaIringa Joseph Ryata akiwa katika soko la Ipogolo alipofanya Ziara katika masoko ya manispaa ya Iringa kwa lengo la kujua namna gani wafanyabisha wanaelimu ya kupambana na Virusi vya Corona
NA FREDY MGUNDA, IRINGA.
WAFANYABIASHA soko la KihesaManispaa ya Iringa wameomba kuwepo na Askari wa Jeshi la akiba katika maeneo yamasoko ili kuwakamata wateja wanaokaidi kwa makusudi agizo la kutakasa mikonoili kujikinga na virusi vya Corona.
Akizungumza mbele ya kaimu meyawa Manispaa ya Iringa na wataalamu wa afya waliotembelea sokoni hapo Mwenyekitiwa soko hilo Subira Mohamedi amesema baadhi ya wateja wanakataa kutumiavitakasa mikono na kuzua hofu ya maambukizi.
Kaimu Meya wa Manispaa yaIringa Joseph Ryata alisema Halmashauri haitosita kuchukua hatua za kisheriaikiwamo kuwafungulia mashtaka, watakaokaidi maagizo ya Wataalamu wa Afyayanayolenga kukabiliana na maambikizi ya corona
“Nimesikitishwa na kitendo cha wananchi kukataa kunawa mikono kwa
sababu hiyo serikali itawachukulia hatua za kisheria kukabiriana na wananchiwanaogoma kutakasa mikono” alisema Ryata
Akiwa katika ziara maalam ya ukaguzi wa mwenendo wa mapamabano ya
kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona katika masoko ya manispaa yaIringa Kaimu Meya wa Manispaa ya Iringa Joseph Nzala Ryata alitembelea soko lakuu jipya la Mlandege,soko la ipogolo na soko la Kihesa, alisema kuwa bado kunahaja kubwa ya kuwaelimisha wananchi juu ya namna bora zaidi ya kujikinga namaambukizi ya corona.
“Bado kunatatizo kubwa na wananchi kutokuwa na elimu ya kupambana
na virusi vya Corona katika Manispaa ya Iringa,hivyo kunahaja ya kutoa elimuendelevu ili wananchi watambue madhara yanayotokana na virusi hivyo” alisemaRyata
Ryata alisema bado kuna mikusanyiko mikubwa isiozingatia umbali
unaotakiwa na wataalamu wa afya wamesema ni miongoni mwa changamoto yenye hatarikubwa pindi maambukizi yanapoibuka.
Hata hivyo hali ni tofauti kabisa katika Soko la Kihesa ambalo
wamefanikiwa kuweka maji na sabuni maeneo yote ya kuingia na kutoka sokoni hapopamoja na maeneo ya ziada wakiwa na lengo mahususi la kujikinga wao wenyewe
Lakini changamoto inayoibukani baadhi ya wateja kukataa kutakasa mikono yao kutokana na wananchi wengi badohawana elimu ya kujikinga na virusi vya Corona.
Kwa Upande wake afisa Afya John Bwire alisema wananchi wote
watakaokaidi kutakasa mikono yao watakabiliwa na adhabu kali kwa mujibu wakisheria za nchi
Aidha katika Ziara hiyo Mganga mkuu wa Manispaa ya Iringa Jesca
Leba alisema wanaendelea na mkakati wa kutoa tahadhari na elimu katika maeneo yoteya mikusanyiko
No comments: