NEWZ ALERT: MKURUGENZI MTENDAJI MTANDAO WA JAMII FORUM MAXENCE MERO AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA AMA KULIPA FAINI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forum Maxence Melo kulipa faini ya Sh. Milioni tatu ama kutumikia kifungo cha mwaka mmoja gerezani baada ya kupatikana na hatia katika kosa la kuzuia jeshi la polisi kufanya kazi yao ya uchunguzi kwa kuzuia taarifa binafsi za wateja wa mtandao wao.

Hukumu hiyo imesomwa leo Aprili 8,2020 na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.

Hata hivyo mahakama imemuachia huru mshtakiwa Micke William ambaye ni Mwanahisa wa mtandao wa Jamii Forum,  baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.
Mshtakiwa Maxence Mello ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa Kijamii wa Jamii Forum akipelekwa chini ya ulinzi baada ya Hakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumkuta na hatia katika kosa la kuzuia jeshi la polisi kufanya kazi yao ambapo amehukumiwa kulipa faini ya Sh. Milioni tatu ama kutumikia kifungo cha mwaka mmoja gerezani.

No comments: