MBUNGE CHADEMA ANG'ATUKA, ATANGAZA KUTOGOMBEA TENA

Charles James, Michuzi TV
MBUNGE jimbo la Bukoba Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfried Lwakatare ang'atuka na kutoa kauli ya kutogombea tena katika Uchaguzi hapa nchini.

Mbunge huyo ametangaza kauli hiyo leo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hotuba ya makadirio ya mapato ya Wizara ya Tamisemi ambapo amewatakia kila heri wabunge wengine.

Tofauti na Komu, Lwakatare yeye hajatangaza kuhamia chama chochote badala yake amesema hatogombea tena katika uchaguzi Mkuu ujao unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.

Akizungumza wakati akiaga amewashukuru wananchi wake kwa imani waliyompatia huku akijisifu kwamba anang'atuka katika nafasi hiyo bila kuwa na madeni yoyote.

"Mimi ni miongoni mwa wabunge wa kwanza wa upinzani ndani ya bunge hili, najivunia kuwa sehemu ya watu waliotoa mchango wao katika kufanikisha siasa za mageuzi nchini. 

Naondoka nikiwa sina deni lolote yaani sidaiwi, na ninajivunia mafanikio makubwa ambayo nimeyaleta katika kipindi changu chote, ni matumaini yangu kwamba mbunge atakayekuja baada ya mimi atafanya zaidi kwa ajili ya wananchi wetu".

Kuondoka kwa Lwakatare kunafanya jumla ya wabunge kutoka Mkoa wa Kagera ambao wametangaza kutogombea tena kufikia wawili ambapo wiki iloyopita Mbunge wa Muleba (CCM), Anne Tibaijuka alitangaza kutogombea katika uchaguzi mkuu ujao.

No comments: