MAFUNDI BINAFSI WA UJENZI WAIPONGEZA SERIKALI KUWAPATIA FURSA
NA MWAMVUA MWINYI, CHALINZE
MAFUNDI binafsi wa ujenzi katika Kitongoji cha Mbukwa Kijiji cha Lugoba, Kata ya Lugoba na Kijiji cha Mbwewe Kata ya Mbwewe Chalinze ,Bagamoyo Pwani, wamesema serikali imewapatia fursa ya ujenzi wa miradi mbalimbali,hali inayowasaidia kujiongezea kipato.
Wakizungumza katika Kitongoji cha Mbukwa na Changarika wilayani hapo, mafundi Rajabu Mdoe na Haruni Mohamed walisema ,hatua hiyo imewapatia pia nafasi ya kuonyesha uwezo na ujuzi wao katika kujenga vyoo na vyumba vya madarasa.
"Serikali ya awamu ya tano inatekeleza mengi na kutetea wananchi wanyonge ,na kwa hili sisi kupewa nafasi kuinua maisha yetu inatusaidia na familia zetu,"
Mdoe anayejenga matundu ya vyoo shule ya Sekondari Changarikwa alieleza kuwa, licha ya hayo, mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha kuchelewesha kufika vifaa vinavyotumika kwa ujenzi, lakini wanatarajia kukamilisha kwa wakati.
Nae Haruni alieleza,anajenga vyumba viwili vya madarasa katika shule mpya ya Mbukwa, na kwamba mbali ya vyumba hivyo tayari ameshakabidhi chumba kimoja alichokikamisha miezi michache iliyopita.
No comments: