Bora useme usaidiwe kuliko kufa na tai shingoni
Na Paul R.K Mashauri
Mara nyingi unapopitia tatizo kubwa katika maisha mfano kupoteza mtu au watu unaowapenda iwe ni mtoto, mume au mke sio jambo ambalo utasahau ndani ya mwaka mmoja. Kuna ambao walipoteza familia zao wakati wa mauaji ya wayahudi yaliyofanywa na Adolf Hitler kule Ujerumani zaidi ya miaka 80 iliyopita lakini mpaka leo vizazi na vizazi havijasahau.

Kuna waliopoteza familia zao wakati wa mauaji ya halaiki ya Rwanda "Rwanda Genocide" zaidi ya miaka 20 iliyopita lakini mpaka leo hawajasahau. Kuna ambao wamepoteza familia zao wakati huu wa COVID-19 na hatujui wanapitia nini.
Kule Italia kwa mfano unakuta mtu amebaki yeye tu. Kapoteza mke, watoto, mashangazi, wajomba nk. Ukivaa viatu vyao utajua ninachozungumza. Hii huleta kitu kinaitwa "Post-traumatic stress disorder (PTSD)"
Dalili za "Post-traumatic stress disorder (PTSD") ni pamoja na "kupoteza-focus mara kwa mara", kukosa usingizi mpaka utumie dawa za usingizi "insomnia", msongo wa mawazo mpaka utumie "depressants" nk. Kuona mauzauza yaani unaona vitu ambavyo havipo mpaka watu wanafikiri "umerogwa" kumbe ni "Post-traumatic stress disorder (PTSD"). Ni mbaya sana usiombe upitie hiyo kitu. Ukipata hili tatizo mtafute "therapist" kwa ajili ya kitu kinaitwa "Cognitive Restructuring" au "Neuro-Linguistic Programming". Usiache iendelee ndani ya ubongo wako. Madhara yake ni kupata ajali, kushindwa kufanya kazi vizuri, kufukuzwa kazi pia mawazo ya kujinyonga "suicidal thoughts"
Nilipewa wimbo huu uitwao "you can Forgive" nilipokumbuka ziara yangu kule Kibondo na Kasulu katika kambi za wakimbizi wa Burundi na Rwanda. Kule nilikutana na kijana ambaye alipoteza familia yake yote, mali zake zote na biashara zake zote. Baadaye nikasoma kitabu kinaitwa LEFT TO TELL cha dada mmoja Mnyarwanda anaitwa Immaculee Ilibagiza ambaye naye alipoteza familia yake wakati wa mauaji ya halaiki nchini Rwanda. Wote hawa walipitia "Post-traumatic stress disorder (PTSD)". Immaculee Ilibagiza alipona haraka "recovery" kwa sababu ya imani yake kwa Mungu. Alipoona wimbo huu alilia.
Kupata "Post-traumatic stress disorder (PTSD)" sio lazima uwe umepitia mauaji ya haraiki "genocide" au uwe mkimbizi. Wapo wanaopoteza watoto wao au ndugu zao pia wakapata hili tatizo. Kila siku unawaza pengine kuna mahala ulikosea ndio maana mtoto wako akaondoka. Ukiona watoto wa wengine unaumia roho nk. Nina kesi ya namna hiyo ambayo mama mmoja "banker" alishindwa kabisa kufanya kazi ikabidi anitafute na mimi kwa sababu sio eneo langu nikampeleka kwa "counsellor" Dr. Chris Mauki.
Inawezekana leo ukawa huna "Post-traumatic stress disorder (PTSD)" lakini huwezi kujua kesho au keshpokutwa. "Nobody knows tomorrow except God". Nimepitia huko ndio maana ninaona ni vyema kuongea na wewe. Nilipopitia "Post-traumatic stress disorder (PTSD)" miaka michache iliyopita nilipata ajali mbaya 3 na sikuwezi kufanya kazi kwa miaka 3 mfululizo. "It was terrible". Nilipopata ajali, sikuwa nimelewa pombe na wala sikuwa najifunza gari lakini sikuwa na uwezo wa ku"concentrate" au kuwa na "focus" nikiwa barabarani. Ilinichukua muda sana ku "recover" kwa sababu wakati huo sikuwa naelewa kuwa napitia "Post-traumatic stress disorder (PTSD)".
Wewe unabahati unasoma mambo haya kwa mtu aliyepitia. Ina maana siku ukipitia tulichopitia sisi utajua kinachotokea na utajua nini ufanye. Mfano, wengine wanapitia "Post-traumatic stress disorder (PTSD)" wakipata kesi mfano kesi za mauaji, kesi za uhujumu uchumi nk. Unaweza ukasikia mtu amefariki ghafla kwa sababu ya presha lakini ukweli ni kwamba presha alikuwa nayo siku zote isipokuwa tatizo analokabiliana nalo linampa sana msongo wa mawazo kiasi kwamba amepata "depression" na matokeo yake ni "Post-traumatic stress disorder (PTSD)".
Mwingine inaweza ikawa ni ugonjwa alionao ambao hana uhakika wa kupona mfano "cancer". Kwa kujua kuwa ugonjwa wake ni mbaya, huyu mtu anaingia katika hatua ya "Post-traumatic stress disorder (PTSD)". Hata kama alikuwa aishi miaka 20 mingine, kwa sababu ya mawazo mengi yanayozunguka kichwani kwake anajikuta akiondoka mapema zaidi kuliko ambavyo ilistahili. Anaanza kuona vitu ambavyo wewe huviona. Unaweza ukasema ni "spiritual" lakini kumbe sio "spiritual" ni tatizo la "Post-traumatic stress disorder (PTSD)". Hii ni kuonyesha tu kuwa tatizo hili linaweza likampata mtu yoyote.
Kuna namna nyingi za kugundua kuwa unaelekea katika "Post-traumatic stress disorder (PTSD)". Ni zipi hizo? Kwanza kabisa unapopata tatizo lolote linalokutia hofu, mashaka au kukushtua na kukupa msongo wa mawazo "stress" unapitia hatua kubwa 4 ambazo ni 1. kukataa "denial" 2. hasira "grief" 3. "depression" 4. "bargaining" 5. "acceptance". Wewe hujawahi kuambiwa fulani amefariki ukakataa mpaka siku ya kuaga ndio ukakubali? Au unaambiwa mke wako kafumaniwa unakataa! Unasema "mama Athumani? Haiwezekani wamekosea jina!
Kwahiyo ukipata tatizo lolote iwe ni ugonjwa, kesi, ndoa jaribu sana kuchunguza uko katika hatua gani. Je ni hatua ya 1. kukataa "denial" 2. hasira "grief" 3. "depression" 4. "bargaining" au hatua ya 5. "acceptance". Hii ni muhimu ili uwe na uwezo wa kujua hapa nahitaji msaada na kweli utafute msaada kabla mambo hayajaharibika. Kwa sababu ukiingia katika "depression" tayari ni tatizo. Ni muhimu sana ukawahi ukiwa katika hatua ya kwanza kabla hujaingia hatua ya pili.
Kwanini nasema ni bora utafute msaada ukiwa katika hatua ya kwanza. Ni kwa sababu ukishaingia katika hatua ya majuto "grief" mara nyingi kuna uwezekano pia wa kupata hasira. Hata ukisikia mtu amemkata viungo vya siri mke wake au mume wake ujue alikuwa katika hatua hii ya pili. Ukipata hasira unaweza ukafanya jambo lolote baya. Na pia ukivuka hatua ya "grief" ukaingia hatua ya "drepression" maana yake ni kwamba uwezo wako wa kufikiria umeathiriwa na msongo wa mawazo. Kwa mantiki hiyo unaweza ukafanya maamuzi au kuapata matatizo ambayo wewe mwenyewe huoni wala huna utambuzi wake. Ndio maana ukifikia hatua hii, wengi hufikiria kukupelea "rehab"-Kigamboni au Bagamoyo.
Swali ni kwanini wengi wanashindwa kuvuka hatua ya kwanza? Ni kwa sababu ya kutokuwa na utamaduni wa kuzungumza "changamoto zetu". Tofauti na jamii za kimagharibu mfano wazungu, Afrika hatuna utamaduni wa kusema yanayotusibu "sharing". Mara nyingi tunaona aibu kusema "nina tatizo". Unawaza watu watanifikiriaje? Na hii ni kwa sababu pia ya kupenda umbeya. Jamii zetu zinapenda sana maneno maneno hasa matatizo ya watu "small talk". Kwahiyo hofu tuliyonayo ni kwamba tukisema basi maneno yatasambaa mji mzima. Ambayo ni kweli. Unamwambia jambo lako mtu kesho unalikuta "group la WhatsApp kama siyo Instagram.
Hii ni tofauti na nchi za kimagharibi ambapo kuna makundi maalum "support groups" kwa watu wanaopitia matatizo. Hakuna wa kumcheka mwenzake wala kumshangaa. Ukipoteza kazi kuna wenzako ambao pia wamefukuzwa kazi wanakutana katika "support group". Umechumbiwa ghafla mume mtarajiwa haonekana kuna wenzako wenye tatizo kama lako nao wanakutana "support group". Kwetu ukitolewa mahari halafu mume akakimbia hakuna wa kukutana nawewe zaidi ya kukutana na maneno mtaana kuwa "unagundu". Ndio maana watu wanakufa na tai shingoni. Kwa sababu mazingira yetu ni ya kupenda kuona watu wana matatizo, wanashindwa, wanadhalilika, wanashitakiwa, wanatumbuliwa, wanasambaratika.
Sasa ufanye nini? Kutokana na hali yetu ni vyema unapogundua kuwa una tatizo ukatafuta mtu unayemuamini sana wa kuzungumza naye. Ukishindwa kabisa basi nenda kwa mtaalam "counsellor" ambaye yeye kwa taaluma yake ni marufuku kutoa siri na akitoa siri yako una uwezo wa kumshitaki kisheria. Anatakiwa awe na usiri "confidentiality". lakini usisahau kuwa yeye pia ni mwanadamu. Kwahiyo unatakiwa uwe na imani kwa Mungu wako. Kumbuka hata mshauri "counsellor" naye anapitia changamoto kama za kwako. Usifikiri kwa sababu mtu ni "counsellor" basi mambo yake shwari. Dunia iache kama ilivyo!
Kwa hiyo kimbilio la pekee ni kwa Mungu wako. Soma Biblia ina mifano mingi sana ya watu waliopitia katika matatizo kama yako lakini mwisho wake waliyashinda na kuishi pasipo "Post-traumatic stress disorder (PTSD)". Kuna Ayubu ambaye alipoteza mali zake zote na magonjwa juu yake. Mke wake akamshangaa, marafiki zake wakamsema na mengine mengi. Lakini Mungu akampa uponyaji na mali maradufu.

Kuna Yusufu ambaye yeye aliuzwa na ndugu zake. Kisha akasingiziwa ametaka kumbaka mke wa Potifa na kuwekwa jela. Lakini Mungu akamtoa na kumpa uwaziri mkuu nchini Misri. Hizi sio hadithi, ni historia ya kweli katika historia ya dunia na ushahidi upo.
Ninachokisema ni kwamba kuna namna nyingi za kuepuka "Post-traumatic stress disorder (PTSD)".Kuna kuongea na watu unaowaamini, Kuna kumuona "counsellor". Lakini kiboko ya yoye, muombe Mungu na soma Biblia. Unapotafakari yote haya sikiliza maneno ya faraja katika wimbo huu wa Paul Mashauri-Faraja@2019
All rights reserved. No part of this article may be reproduced, distributed, or transmitted in any form or by any means including photocopying, recording or other electronic or mechanical methods, without the prior written permission of the author. You can contact the author through ceo@masterclassworldwide.co.tz or Tel: +255 714 508508-Paul R.K Mashauri.

No comments: