WCB Yathibitisha Rasmi Kuachana na Harmonize
Harmonize moyo wake haupo WCB ila kimakaratasi Harmonize bado yupo WCB, na ameshaandika barua ya kuvunja mkataba na WCB na kufuata taratibu zote za kisheria.“Hili jambo si sawa kulingana na maudhui ya tamasha hilo. Maudhui ya Wasafi Festival ni umoja. Msanii akiamua kuacha kuambatana na wasanii wenzake ambao wapo pamoja katika tamasha ni kwenda kinyume.
“Sisi katika tamasha letu hatupendi kutengeneza matabaka, tumeamua kuwa kitu kimoja, siyo kwamba Diamond, Rayvany hawakuwa na uwezo wa kutumia usafiri wao binafsi kama alivyofanya Harmonize.
“Harmonize ameshatuma barua ya maombi Wasafi kuvunja mkataba wake na yupo tayari kufuata sheria zote. Sisi tumependezwa na hatua yake kwa sababu labda kuna vitu ameona akivifanya atafika mbali,” amesema Sallam.
Sallam ameongeza kuwa wanashukuru kwa uungwana aliouonyesha wa kufuata taratibu zote za kisheria kuhusu kuvunja mkataba wake, na wao kama menejimenti watakaa kujadili ombi lake.
Alipoulizwa kuhusiana na Kampuni ya Zoom Production ambayo inamilikiwa na Harmonize akiwa na ubia na Diamond Planumz, Sallam amesema kuwa
” Zoom iliundwa nje ya kampuni ya WCB na ni mali ya Harmonize na Diamond Platnumz, kwa hiyo itabaki kuwa hivyo, hawa watu hawajagombana na wataendelea kufanya kazi pamoja,” amesema Sallam Sk.
Kwa muda mrefu kulikuwa na tetesi kuhusu Harmonize kuachana na Lebo hiyo ya WCB lakini hakutaka kuliweka wazi, japokuwa ishara za yeye kujiondoa WCB alianza kuzionyesha mapema hasa baada ya kuanzisha ‘Lebo’ yake inayoitwa Konde Gang, na kufuta utambulisho wa ‘Signed Under WCB Label’ kwenye ukurasa wake wa Instagram.
The post WCB Yathibitisha Rasmi Kuachana na Harmonize appeared first on Global Publishers.
No comments: