WAZIRI KABUDI AMUAGA MRATIBU MKAZI WA UMOJA WA MATAIFA NCHINI, AKUTANA NA WANAHABARI NA APOKEA UJUMBE WA WAENDESHA BAISKELI


Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akizungumza katika hafla fupi ya kumuaga Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez iliyofanyika hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam.

Waziri Kabudi katika hotuba yake amempongeza Bwana Rodriguez kwa utumishi wake uliotukuka katika kipindi chote akiwa nchini. Aidha, amemshukuru kwa kushirikiana na Serikali na kujitoa kwa dhati katika kuchangia juhudi kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanywa Serikali nchini.

Bwana Rodriguez amemaliza muda wake wa kuhudumu nchini Tanzania ambapo amefanya kazi kwa kipindi cha miaka mitano.
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Kulia) na Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, anayemaliza muda wake wa kuhudumu nchi wakifurahia jambo wakati wa hafla fupi ya kumuaga
Bw. Deusdedit Kaganda Kaimu Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa akizungumza kwenye hafla fupi ya kumuaga Bw. Rodriguez Maratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini ambaye amemaliza muda wake wa kuhudumu nchini 
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kulia) na Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini wakishirikishana jambo  wakati wa hafla hiyo
Bi.Ramla Khamis Afisa Mambo ya Nje Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza katika hafla ya kumuaga Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kulia) akikabidhi zawadi kwa Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini ambaye amemaliza muda wake wa kuhudumu
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Bw. Alvaro Rodriguez Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini ambaye amemaliza muda wa kuhudumu wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi kutoka wizarani na Ofisi ya Umoja wa Mataifa.
Mhe. Prof. Paramagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Waziri Kabudi katika Mkutano wake na wanahabari amewashukuru nakuwapongeza waandishi wa habari na vyombo vya habari, kwa ushirikiano mkubwa na uzalendo waliouonyesha katika kuutangaza Mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Waziri Kabudi alitumia fursa hiyo kutoa rai kwa waandishi wa habari kuendelea kufuatilia na kuuhabarisha umma masuala mbalimbali yanayojiri kweny ya Jumuiya SADC.

Tanzania itaendelea kuwa mwenyeji wa Mikutano mbalimbali ya kisekta ya SADC katika kipindi cha hiki cha mwaka mmoja cha Uenyekiti wake.
Bw. Emmanuel Buhohela Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza wakati wa Mkutano na Wanahabari uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Agosti 21, 2019. 
Bibi Agnes Kayola Kaimu Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda akizungumza wakati wa Mkutano na waandishi wa habari 
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano 
Meza kuu ikifuatilia Mkutano uliokuwa ukiendelea.

Wakati huohuo Waziri Kabudi amepokea ujumbe wa wawaendesha baiskeli unaojumuisha washiriki kutoka nchi wanachama wa Jamuiya ya Afrika Mashariki. Ziara hii ya waendesha baiskeli imeandaliwa na asasi ya kiraia "Camp fire" ya nchini Uganda. Ziara yao inahusisha kuzunguka nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa lengo la kukuza umoja na ushirikiano wa kikanda.

Akizungumza kiongozi wa waendesha baiskeli hao bwana John Balongo ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapa ushirikiano na mapokezi mazuri katika kipindi chote walichokuwa nchini. 
Msafara wa waendesha Baiskeli wakiwasili katika viunga vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Agosti 21, 2019 
Waziri Kabudi akisalimiana na ujumbe wa waendesha baiskeli kutoka nchi wanachama za Afrika Mashariki walipowasili katika viunga vya Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere 
Waziri Kabudi akimkabidhi bendera ya Taifa mwakilishi wa Tanzania katika ziara ya baiskeli ya Afrika Mashariki, mara baada ya kuwapokea katika viunga vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam 
Waziri Kabudi akizungumza wakati wa mapokezi ya msafara wa ujumbe wa waendesha baiskeli wa Afrika Mashariki 
Bw. Eliabi Chodota, Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii (mwenye tai nyekundu) Wizara ya Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akizungumza wakati wa mapokezi ya msafara wa waendesha baiskeli kutoka nchi wanachama wa Afrika Mashariki 
Bw. John Barongo, Kiongozi wa msafara wa waendesha baiskeli wa Afrika Mashariki akizungumza baada ya mapokezi 

Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchi za Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa waendesha baiskeli 




No comments: