VIDEO: Vodacom Yamwaga Bil 9 Kudhamini Ligi Kuu

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom jana Agosti 23, 2019 wamesaini Mkataba wa miaka 3 wa Udhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Mkataba huo unathamani ya shilingi bilioni 9 ambapo kila mwaka shilingi bilioni 3.

 

Katika hafla hiyo, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, amelitaka Shirikisho hilo kuzingatia masharti yaliyopo kwenye mkataba wa udhamini.

 

Ameongeza kuwa soka la Tanzania litaendelea kukua kwa viongozi kuwa makini kama walivyo viongozi wa sasa, kwani hakuna mwekezaji aliyetayari kusaini mkataba na watu wa hovyo.

The post VIDEO: Vodacom Yamwaga Bil 9 Kudhamini Ligi Kuu appeared first on Global Publishers.

No comments: