Tunda akiwa penzini ni kujifungia

PENZI ni tamu kama asali! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya video queen, Tunda Sebastian kueleza kuwa akiwa katika mapenzi mazito hatamani kabisa kutembeatembea na mpenzi wake bali kazi yao inakuwa ni moja tu kujifungia ndani.  Tunda aliliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa tatizo lake ni moja kuwa akiingia kwenye mapenzi anaingia na miguu yote miwili na mwili wake wote ndiyo maana kuna wakati watu wanamuona kama kichaa.

“Nikiwa kwenye uhusiano wa kimapenzi ukweli napenda sana kujifungia ndani tu muda wote na ndiyo maana mimi na mppenzi wangu Whozu hamtuoni sehemu tofautitofauti kwa sababu mara nyingi tunajifungia ndani tu, huo ndiyo ugonjwa watu nikiingia kwenye uhusiano,” alisema Tunda.

The post Tunda akiwa penzini ni kujifungia appeared first on Global Publishers.

No comments: