SILVIA ALIVYOTWAA TAJI LA MISS TANZANIA 2019

Mrembo Silvia Sebastian mkazi wa Buhongwa  jijini Mwanza (katikati) akiwapa ‘hi’ wageni waalikwa baada ya kutwaa taji la Miss Tanzania usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam.

Mrembo Silvia Sebastian mkazi wa Buhongwa Mwanza ambaye pia alitwaa taji la Miss Mwanza na Miss Lake Zone mwaka huu usiku wa kuamkia leo ametwaa taji la Miss Tanzania katika kinyang’anyiro kilichowashirikisha warembo ishirini kutoka mikoa na kanda mbalimbali hapa nchini.

Warembo wakitoa shoo.

Kinyanganyiro hicho kilifanyika Jengo la LAPF Tower Kijitonyama Dar na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa mashindano akiwemo waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe.

 

Sambamba na Mwakyembe ambaye alikuwa ndiye mgeni rasmi pia alikuwepo Waziri wa Utalii mstaafu, Waziri Lazaro Nyarandu.

Silvia katika vazi la jioni kabla ya kutangazwa mshindi. 

The post SILVIA ALIVYOTWAA TAJI LA MISS TANZANIA 2019 appeared first on Global Publishers.

No comments: