AZAM: TUTACHUKUA MAKOMBE MATATU MSIMU HUU
HUENDA huu ukawa msimu wa kipekee kwao licha ya kwamba, tayari wameshuhudia wakiyakosa mataji mawili kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/20. Wanaozungumziwa hapa ni Azam FC ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2013/14.
Wikiendi iliyopita, Azam ilifungwa mabao 4-2 na Simba katika Ngao ya Jamii, pia mwezi uliopita ilifungwa bao 1-0 na KCCA ya Uganda katika mchezo wa fainali ya Kombe la Kagame 2019.
Azam FC iliyoanza kushiriki Ligi Kuu Bara mwaka 2008, leo Jumamosi itakuwa na mechi ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Fasil Kenema ya Ethiopia. Mechi hiyo ni ya marudiano. Katika mchezo wa kwanza uliochezwa wiki mbili zilizopita nchini Ethiopia, Azam FC ilifungwa bao 1-0.
Kesho itakuwa nyumbani kwenye uwanja wao wa Azam Complex jijini Dar es Salaam. Msimu uliopita katika Ligi Kuu Bara, Azam FC walimaliza nafasi ya tatu, huku wakiibuka mabingwa wa Kombe la Shirikisho (FA) na kutwaa Kombe la Mapinduzi. Mataji hayo iliyatwaa chini ya makocha wa muda, Meja Mstaafu, Abdul Mingange na Idd Nassor Cheche waliochukua mikoba ya Hans van der Pluijm na Juma Mwambusi.
Msimu huu, Azam FC itakuwa chini ya Kocha Etienne Ndayiragije raia wa Burundi, huku Mingange na Cheche wakiwa wasaidizi wake.
Kuelekea kwa msimu huu wa Ligi Kuu Bara ambapo mechi zake zinatarajiwa kuanza kuchezwa kesho Jumamosi, Championi Ijumaa limefanya mahojiano na Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdukarim Amin Popat ambaye anafunguka mambo kadhaa yanayohusu timu hiyo. USAJILI “Katika
Wanataka kufika makundi Kombe la Shirikisho Afrika usajili, tumewaongeza wachezaji watano tu, lakini kwenye usajili huo haukukamilika kama ambavyo tulitaka kwa sababu kocha kuna aina ya wachezaji aliwahitaji, lakini hawakupatikana.
“Kwenye usajili huo, upande wa wachezaji wa kimataifa tumesajili watatu ambao ni Richard Djodi kutoka Ghana na Seleman Ndikumana anayetokea Burundi kama ilivyo kwa Emmanuel Mvuyekure.
“Wa hapa ndani tumemchukua Kassim Khamis na Iddy Seleman ‘Nado’. “Kuna wachezaji ambao wameondoka kwa sababu mbalimbali ikiwemo kumaliza mikataba yao. Miongoni mwao ni Ramadhan Singano, Ismail Gambo, Joseph Kimwaga, Enock Atta Agyei na Metacha Mnata.
HALI YA KIKOSI “Wachezaji wetu wana ari ya kumbana na hamu ya kutwaa mataji ndiyo maana unaona wanapambana hata katika mechi za maandalizi.
“Tuna wachezaji wenye uwezo ambao wakiweka bidii zaidi, watafika mbali. “Tumecheza mechi nyingi za kirafiki kabla ya kuanza kwa msimu huu, lengo ni kuangalia uwezo wa wachezaji wetu.
Miongoni mwa mechi hizo ni dhidi ya Namungo, Polisi Tanzania na Agle Noir. “Pia tumecheza mechi za mashindano kuanzia michuano ya Kagame, lakini pia ile ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Fasil Kenema pamoja na Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.
KAMBI “Suala la kambi ya maandalizi tuliipata kipaumbele, lakini ratiba haikuwa rafiki sana kwa sababu tumetoka kwenye ligi hatujapumzika, baadhi ya wachezaji wakaenda kushiriki michuano ya Afcon, waliporudi michuano ya Kagame ikaanza.
“Hatujapumzika vizuri, ratiba ya michuano ya kimataifa ikaja na tukaenda Ethiopia kucheza mechi yetu ya kwanza. “Hapo unaona jinsi ratiba ilivyokuwa ngumu na ilimpa shida kocha wetu Etienne.
MAJERUHI “Kwenye maandalizi yetu tumepata changamoto ya majeruhi ambao kwa namna moja au nyingine wameathiri programu za kocha. “Mchezaji wetu kama Aggrey Moris amekuwa nje kwa muda mrefu na alipata matatizo akiwa na kikosi cha Taifa Stars, hivyohivyo kwa Mudathir Yahaya. Kwa hali hii unakuta kocha anawakosa baadhi ya wachezaji wake kwenye michezo ya mwanzo wa ligi.
MIPANGO YAO “Mipango yetu kama klabu ni kuona klabu inafanikiwa kufanya vizuri kwenye ligi bila ya kuhofia timu yoyote ile kwa sababu tupo vizuri.
“Tunataka kupambana na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, FA na hata Kombe la Mapinduzi, tunataka kufanya hivyo na hayo ndiyo malengo yetu makubwa kama klabu ambayo tumejiwekea. “Tayari tumekosa makombe mawili, lile la Kagame na Ngao ya Jamii, hivyo nguvu zetu tumezielekeza huko.
“Kocha wetu ana mipango yake, lakini kikubwa msimu huu kwetu tunataka uwe wa kipekee kwa kuandika rekodi tofauti kwenye michuano ambayo tutashiriki. “Pia kimataifa tunacheza mechi ya marudiano na ile timu ya Ethiopia (Fasil Kenema) hapa lengo ni kupata ushindi na malengo yetu ni kufika hatua ya makundi kwanza ndiyo mambo mengine yaweze
The post AZAM: TUTACHUKUA MAKOMBE MATATU MSIMU HUU appeared first on Global Publishers.
No comments: