ASKOFU SHOO ACHAGULIWA TENA KUONGOZA KANISA LA KILUTHERI NCHINI
Askofu Dkt. Frederick Shoo ametangazwa mshindi usiku wa kuamkia leo dhidi ya wagombea wengine na ataongoza Kanisa hilo kwa kipindi kingine cha miaka minne (2019-2023).
Askofu Shoo amepata kura 144 huku mshindani wake wa karibu, Dkt. Keshomshahara akipata kura 74 kati ya kura 218 zilizopigwa katika mzunguko wa mwisho baada ya kubaki wao wawili.
Awali, katika kinyang’anyiro hicho alichuana na Maaskofu wenzake wakiwemo Dkt. Steven Munga, Dkt. Abednego Keshomshahara, Blaston Gavile na Dkt. Alex Malasusa (Aliyewahi kuongoza Kanisa hilo katika cheo hicho kwa miaka 8).
Dkt. Shoo alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuongoza Kanisa hilo Agosti mwaka 2015 baada ya kupata kura 153, dhidi ya Dkt. Munga aliyepata kura 67 wakati huo
The post ASKOFU SHOO ACHAGULIWA TENA KUONGOZA KANISA LA KILUTHERI NCHINI appeared first on Global Publishers.
No comments: