Safari ya Kwanza ya Air Tanzania kutoka DAR – MUMBAI Yazinduliwa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Injinia Isaack Kamwelwe akikata utepe wakati wa hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa safari ya Mumbai nchini India kwa ndege ya Air Tanzania ikiwa ni safari ya kwanza kwa ndege za Air Tanzania kutoka nje ya Bara la Afrika na ni safari ya moja kwa moja kutokea Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Ndege ya kwanza ya Air Tanzania imeondoka Julai 17, 2019 kuelekea Mumbai, nchini India.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Injinia Isaack Kamwelwe akikata keki wakati wa hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa safari ya Mumbai nchini India kwa ndege ya Air Tanzania ikiwa ni safari ya kwanza kwa ndege za Air Tanzania kutoka nje ya Bara la Afrika na ni safari ya moja kwa moja kutokea Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.Ndege ya kwanza ya Air Tanzania imeondoka Julai 17, 2019 kuelekea Mumbai, nchini India.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandishi Isack Kamwelwe jana, Jumatato, Julai 17, 2019 amezindua safari ya kwanza ya kimataifa ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) ya kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Mumbai India.
Waziri Kamwelwe amezindua safari hiyo, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwenye jengo jipya la safari za kimataifa ‘Terminal 3’ ambalo linatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.
Katika hafla hiyo Waziri Kamwelwe amewapongeza Watanzania wote ambao wamekuwa waaminifu kulipa kodi kwa serikali, akisema ndio waliowezesha ununuzi wa ndege 6 za shirika hilo na ujenzi wa jengo hilo jipya.
“Ni jitihada zenu kwenye ulipaji kodi ndizo zimewezesha kufikia mafaniko haya makubwa pamoja na mengine mengi yanayokuja, ni lazima mjipongeze,” ameeleza.
Ameongeza kuwa safari za kimataifa zitasaidia sana katika kukuza biashara na uwekezaji nchini, kuongeza shughuli za utalii, kuunganisha nchi na wananchi wake na mataifa mengine duniani, kukuza uchumi na kuboresha maisha ya Watanzania.
The post Safari ya Kwanza ya Air Tanzania kutoka DAR – MUMBAI Yazinduliwa appeared first on Global Publishers.
No comments: