Tigo Yawakabidhi Tiketi Washindi wawili Kushuhudia AFCON
Kupitia droo ya pili ya promosheni ya SOKA LA AFRIKA, kampuni ya Tigo imewatangaza washindi wengine wawili na kuwakabidhi tiketi za kwenda kushuhudia michuano ya Mataifa ya Afrika yanayofanyika nchini Misri na kufanya idadi ya washindi kuwa watano.
Washindi walioshinda tiketi katika droo ya pili ni Sanga Massawe kutoka Moshi Kilimanjaro na Emmanuel Mushi kutoka Dar es Salaam.
Mapema wiki iliyopita, Tigo iliwakabidhi tiketi washindi watatu katika droo ya kwanza ya promosheni hiyo. Washindi wa droo ya kwanza ni Kalaghe Rashid na Godfrey Muta kutoka Dar es Salaam na Rehema Kassim kutoka Tanga.
Kupitia Promosheni ya Soka la Afrika, wateja wa Tigo wanayo nafasi ya kujishindia safari ya kwenda Misri kushuhudia michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika pamoja na fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 50.
Kupitia promosheni hii, wateja 10 wa Tigo wataweza kujishindia tiketi za kwenda kushuhudia mashindano haya makubwa barani Afrika, ambapo timu ya taifa, Taifa Stars nayo itakuwa inashiriki kwa mara ya kwanza baada ya miaka 36.
Ili wateja waweze kushiriki katika promosheni hii ya SOKA LA AFRIKA na kujipatia nafasi ya kuwa mamilionea pamoja na kushinda tiketi, watatakiwa kutuma neno SOKA kwenda 15670 au kutembelea tovuti ya www.tigosports.co.tz ili kuweza kujibu maswali yanayoihusu mashindano hayo yanayofanyika nchini Misri.
SOKA LA AFRIKA ipo mahususi kwa ajili ya kuwazawadia wateja waaminifu wa Tigo ambao siku zote wamekuwa mstari wa mbele kutumia bidhaa na huduma za kampuni hiyo.
Fainali za Mataifa ya Afrika, ni mashindano makubwa kuliko yote barani Afrika ambayo yanawaleta pamoja wachezaji wa Kiafrika wanaoshiriki ligi kubwa na zenye ushindani ndani na nje ya bara la Afrika.
Zaidi ya wateja mia moja watashinda fedha kila siku, kila wiki na kila mwezi kwa muda wa miezi mitatu na kadiri mteja anapojibu maswali, ndivyo anavyozidi kujiongezea pointi na nafasi kubwa zaidi ya kushinda tiketi kwenda Misri au mamilioni ya pesa.
The post Tigo Yawakabidhi Tiketi Washindi wawili Kushuhudia AFCON appeared first on Global Publishers.
No comments: