STARS KUCHANGIWA LEO JIJINI DAR

ZOEZI la kuichangia Taifa Stars ili ifanye vizuri kwenye Afcon inayoanza kesho, linafikia tamati leo Alhamisi katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam  huku Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa mgeni rasmi.

 

Akizungumza na Spoti Xtra Waziri Mwakyembe amewataka Watanzania kwa jumla kuungana katika hafla hiyo ambayo chochote kitakachopatikana kitakwenda moja kwa moja kwenye mifuko ya wachezaji. Hafla hiyo itaanza saa 4 asubuhi mpaka jioni.

 

“Hiki tunachokifanya ni sehemu ya uzalendo kuonyesha kuwa tupo pamoja na wanajeshi wetu watakaokuwa wanapambania heshima ya nchi yetu kule Misri.

 

“Pesa tunayochangisha inakwenda moja kwa moja kwenye mifuko ya wachezaji kwa sababu mambo mengine yote yameshafanyika, kama sehemu ya kulala, chakula na posho ndogo ndogo hivyo vyote serikali imeshafanya, lakini hii inakwenda kuwahamasisha ili wajue kuwa hawapo peke yao katika mapambano hayo,” alisema Mwakyembe.

 

Naye Mkurugenzi wa Maendeleo Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Yusuph Singo aliliambia Xtra kuwa; “Maandalizi yote yapo vizuri na muitikio ni mkubwa sana.”

The post STARS KUCHANGIWA LEO JIJINI DAR appeared first on Global Publishers.

No comments: