YONDANI AFUNGUKA KUTOMPA MKONO AJIBU

BEKI mkongwe wa kati wa Yan­ga, Kelvin Y o n d a n i amefuta ukimya na kufungukia ishu yake ya kutopeana mkono na nahod­ha wake, Ibrahim Ajibu.

 

Hiyo, ikiwa ni siku moja tangu iibuke taarifa za wachezaji hao kutokuwepo ka­tika mahusiano mazuri baada ya video kusambaa ya Yondani kukataa kumpa mkono Ajibu.

 

Kitendo hicho kili­tafsiriwa na wengi kuwa Yondani ana kinyongo na Ajibu, baada ya ku­vuliwa unahodha na mikoba yake kukabidhi­wa kiungo huyo.

Tukio hilo la aina yake lilitokea wakati Ajibu akiwatam­bulisha wachezaji wake kwa mgeni rasmi wakati Yanga ilipocheza mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba juzi, Dar.

 

Akizungumza na Championi Ju­matatu, Yondani alisema hakuna bifu lolote kati yake na Ajibu huku akitaja uchochezi wa mashabiki ndiyo ume­sababisha minong’ono kuhusu tukio hilo.

 

Yondani amedai kuwa ha­kumpa mkono Ajibu kama masi­hara tu, kwa kuwa siyo utaratibu wa nahodha kushikana mikono na wachezaji wakati akiwatam­bulisha.

 

“Mimi Ajibu ni mdogo wangu na mara nyingi tumekuwa tuki­taniana ndani na nje ya uwanja na hilo tukio la mimi kukataa mkono wa Ajibu nilijua ni masi­hara ananiletea, ndiyo maana nikakataa kumpa mkono.

 

“Kwa sababu Ajibu katika mechi zote za ligi ambazo tume­zicheza hajawahi kutupa mikono wachezaji, yeye anaishia kutut­ambulisha majina yetu na mgeni rasmi ndiyo anatupa mikono, hivyo nashangaa suala hilo lina­vyochukuliwa.

“Kama ningekuwa na bifu au chuki na Ajibu, basi nisingekuwa nampa ushauri na siyo huyo, wachezaji wengi wanafuata ush­auri kwangu kutokana na ukong­we nilionao wakiwemo baadhi Samatta (Mbwana), Msuva (Si­mon) na Banda (Abdi), hivyo niwaondoe hofu mashabiki wa Yanga katika hilo, mimi sina ugo­mvi na Ajibu,” alisema Yondani.

 

Championi Jumatatu, lilimtafuta Ajibu kuzun­gumzia hilo simu yake iliita bila kupokelewa lakini taarifa iliy­osambaa kwenye mitandao ya kijamii ambayo haijathibitishwa kama ni ya Ajibu, inamnukuu hivi:

 

“Nahisi wenzangu walinis­hangaa kuwatambulisha kwa kuwashika mkono, mara nyingi huwa hatufanyagi hivyo, Yon­dani ni kaka yangu na siyo yeye pekee pia Dante (Andrew Vice­nt), Yondani alisita na kuniam­bia hii mpya. Sina shida na kaka yangu huyu, sisi ni wadogo zake na mengi tunajifunza kwake.”

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam.

The post YONDANI AFUNGUKA KUTOMPA MKONO AJIBU appeared first on Global Publishers.

No comments: