WAVUVI TOENI HOFU SERIKALI INASHUGHULIKIA MATATIZO YENU
NAIBU waziri wa mifugo na uvuvi nchini Abdullah Ulega amewataka wavuvi nchini kutokuwa na hofu katika shughuli zao za uvuaji wa samaki katika bahari maziwa na mito.
Rai hiyo ameitoa jana alipokuwa akizungumza na wavuvi wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani katika mwendelezo wa ziara zake nchini kwa kusudi la kuwaelimisha wavuvi kile kinachofanywa na serikali ya awamu ya tano.
Alisema kuwa serikali ilichukua hatua kali za kuchoma nyavu ambazo zilikuwa ni hatari kwa kizazi na masalia ya viumbe hao.
"Nendeni mkafanye kazi za uvuvi bila kuwa na wasiwasi ila sheria kanuni na taratibu zifuate hakutokuwa na kiongozi wa aina yeyote ile atakayewasumbua "Alisema Ulega.
Aidha aliongeza kuwa kwa wale wote waluochukuliwa jenereta zao taa za kuvulia zjmeamuliwa zirudishwe kwa wavuvi hao mara moja kwani serikali imeamua virudishwe haraka sana,kuhusu faini wanazopigwa wavuvi ni kwa mujibu wa she ria za mazingira.
Mbali na hayo Ulega amewataka wavuvi hao kufanya kazi zao bila uoga kwani kipindi hiki cha hapa kazi tu kimejikita katika kuhakikisha wananchi wake wanyonge wanakuwa na kipato cha kati ili kujiondoa katika umasikini.
Kwa upande wake Juma Hassan mbaye ni mvuvi kutoka wilayani Bagamoyo ameipongeza serikali kupitia naibu waziri huyo kwa ufafanuzi mkubwa alioutoa kuhusu uvuvi haramu ulivyokuwa ukididimiza maendeleo ya taifa let kwa kipindi kirefu.
Naye mkuu wa wilaya hiyo zainabu kawawa amewataka wananchi kuwa na subra kwani serikali inayafanyia kazi malalamiko ya wavuvi na hasa waliokamatiwa nyavu zao .
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdullah Ulega akingalia baadhi nyavu hatari kwa kizazi na masalia na viumbe hai zilizokamatwa katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdullah Ulega akizungumza na wavuvi pamoja na wananchi wa kijiji cha Mligotini wilaya Bagamoyo mkoa wa Pwani.ambapo aliwaomba kufanya kazi bila kuwa na wasiwasi ila sheria kanuni na taratibu zifuatwe,
Semu ya sabuni pamoja na mafuta yanayo tengenezwa kwa zao la Mwani
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,Zainabu Kawawa akizungumza na wavuvi pamoja na wanchi wa wila hiyo ambapo amewaomba kuwa na subra kwani serikali inayafanyia kazi malalamiko ya wavuvi na hasa waliokamatiwa nyavu zao .
Wavuvi pamoja na wanachi wa wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdullah Ulega.
No comments: