Watu 34 washikiliwa na Polisi mkoani Mbeya kwa tuhuma mbalimbali
JESHI la polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu 34 kwa tuhuma mbalimbali na hiyo ni baada ya kufanyika kwa misako katika maeneo mbalimbali katika Mkoa wa Mbeya na makosa hayo ni pamoja na:
Kukamatwa kwa pombe ya moshi ( gongo) ambapo jeshi la polisi mkoani humo limeeleza kuwa mnamo tarehe 17 februari mwaka huu majira ya saa tano asubuhi katika kata ya Nkuyu tarafa ya Unyakyusya, Wilayani Kyela polisi walimkamata Hohn Mwaseba (31) mkazi wa Nkuyu akiwa na pombe ya haramu ya moshi yenye ujazo wa lita 13 uchunguzi unaonesha mtuhumiwa ni muuzaji wa pombe hiyo na upelelezi unaendelea.
Katika hatua nyingine jeshi la polisi Mkoani humo limemkamata Prisca Peter (32) kwa tuhuma za kuingiza bidhaa nchini bila kibali, imeelezwa kuwa mnano tarehe 16 Februari majira ya saa tatu usiku jeshi la polisi lilimkamata mtuhumiwa akiwa na pombe aina ya Prince chupa 20, kinywaji cha Power chupa 60, maziwa aina super shake chupa 12, na biskuti aina ya chiko dazani 2 ambazo hazikulipiwa ushuru akiwa anazisafirisha kwa usafiri wa coaster kutika Tunduma kwenda Kyela na chanzo cha tukio hilo imeeleza kujipatia kipato kikubwa kwa kukwepa kulipa kodi na mtuhumiwa amekiri kutenda makosa hayo na upelelezi unaendelea na baadaye mtuhumiwa kufikishwa mahakamani.
Katika tukio jingine jeshi la polisi Mkoani humo katika eneo la Kalumbulu Wilayani Kyela lilimkamata Stewart Ntulo akiwa na lita 60 za mafuta ya Cook well bidhaa iliyokuwa inaingizwa nchini kutoka nchi jirani ya Malawi bila kibali na upelelezi unaendelea.
Vilevile jeshi la polisi limeeleza kuwa usiku wa tarehe 15 mwezi huu katika kata ya Tembela wilaya ya kipilisi ya Mbalali jeshi la polisi liliwakamata watuhumiwa kadhaa kwa tuhuma za kumjeruhi Majuto Mahowe (32) mkazi wa Ifiga kwa kumtuhumu ameiba mtoto.
Aidha jeshi la polisi Mkoani humo linawashikilia watu 18 kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko kinyume na taratibu huko katika kataa ya Itagano tarafa ya Sisino jijini Mbeya.
Wakati huo huo jeshi la polisi linamshikilia Joshua Frank (32) kwa kukutwa na mali zinazosadikika kuwa ni za wizi, maali hizo ni pamoja na printer kubwa 2 aina ya Epson, laptop 2 ( Accer na Fujistu) na vifaa vingine vingi vya umeme na upelelezi unaendelea kabla ya mtuhumiwa kufikishwa mahakamani.
No comments: