WASICHANA WATATU NA MMOJA KATI YA WAVULANA SABA WAFANYIWA UKATILI WA KINGONO KABLA YA MIAKA 18

Takwimu za vitendo vya ukatili kwa watoto nchini  vinaonyesha kuwa mmoja kati ya wasichana watatu na mmoja kati ya wavulana saba hufanyiwa ukatili wa kingono kabla ya kufikisha miaka 18.

Alisema hayo Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii anyeshughulikia masuala ya malezi kwa watoto na familia  Grace Mwangwa wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Mikoa ya Shinyanga, Katavi na Kigoma Mapema leo katika mji mdogo wa Kasulu Mkoani Kigoma.

Mafunzo hayo kwa Maafisa hao yafanyika Mjini kasulu kwa lengo la kuwapatia mafunzo ya Kitini cha Elimu ya Malezi ya Familia kwa Watoto na kuwawezesha  kupata mbinu na uwezo wa kuwajengea  wazazi na walezi maarifa na washiriki hao wanatoka kwenye Mikoa yenye kiwango kikubwa cha mimba na ndoa za utotoni.

Aidha Bi. Mwangwa aliwambia wajumbe wa mafunzo hayo kuwa viwango vya ukatili wa kimwili ni asilimia 72 kwa wasichana na asilimia 71 ni wavulana ambavyo vinasababishwa zaidi na wazazi, walezi wakiwemo  walimu.

Bi. Mwangwa alisema pia kuwa  robo tatu ya watoto huadhirika zaidi na ukatili wa kihisia kutokana na kutukanwa matusi, kubaguliwa na kupuuzwa akiongeza kuwa Vitendo vyote hivi vinasababishwa na desturi na kanuni za jamii zenye madhara na zinazounga mkono kutumia ukatili katika kumlea mtoto.

‘’Ukosefu wa uelewa, maarifa na stadi zinazohusu njia za malezi zisizo za ukatili na umma kutoelimishwa vya kutosha kuhusu haki za mtoto pamoja na umaskini wa kaya unaosababisha wazazi au walezi kuwatelekeza watoto, uhamiaji kutoka vijijini kwenda mijini ambapo watoto hutolewa vijijini na ndugu zao kwa ahadi za maisha mazuri na kudhoofika kwa mifumo ya asili ya kijamii. Alisikika akisema Bi. Mwangwa.

Aliwaambia washiriki wa kikao hicho kuwa nafahamu dhihiri kuwa,mfumo wa ulinzi wa mtoto ni msingi imara ambao unapelekea uwekaji wa mazingira ya ulinzi kwa watoto wetu kuanzia ngazi ya taifa,jamii na familia kwa ujumla.

Bi. Mwangwa aliendelea kusema kuwa serikali kwa kushirikiana na wadau imedhamiria kushughulikia ukatili dhidi ya watoto kwa kuweka sera, sheria na mipango inayolenga kulinda haki za mtoto.

Kupitia Kitini hiki cha Elimu ya Malezi ya Familia kwa Watoto washiriki  watapata mbinu na kuwa na uwezo wa kuwajengea  wazazi/ walezi maarifa na stadi  juu ya mikakati ya kijamii ya kuzuia aina  zote za ukatili dhidi ya watoto kupitia elimu madhubuti ya malezi chanya yanayofaa katika jamii.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii anyeshughulikia masuala ya malezi kwa watoto na familia Grace Mwangwa pamoja na Kaimu Afisa Maendeleo wa Mkoa wa Kigoma Bw. Msafiri Nzunuri  wakifuatilia jambo  wakati wa mafunzo kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Mikoa ya Shinyanga, Katavi na Kigoma Mapema leo katika mji mdogo wa Kasulu Mkoani Kigoma.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii anyeshughulikia masuala ya malezi kwa watoto na familia Grace Mwangwa akitoa maelekezo wakati wa  ufunguzi wa mafunzo kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Mikoa ya Shinyanga, Katavi na Kigoma Mapema leo katika mji mdogo wa Kasulu Mkoani Kigoma.
 Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii anyeshughulikia masuala ya malezi kwa watoto na familia Bw. Emmanuel Burton akitoa mada wakati wa mafunzo kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Mikoa ya Shinyanga, Katavi na Kigoma Mapema leo katika mji mdogo wa Kasulu Mkoani Kigoma.
Baadhi ya Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Mikoa ya Shinyanga, Katavi na Kigoma wakifuatilia kwa makini mafunzo ya Kitini cha Elimu ya Malezi ya Familia kwa Watoto yanayotolewa na Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii leo katika mji mdogo wa Kasulu.

No comments: