MWANARIADHA FAILUNA AFANIKIWA KUTETEA NAFASI YAKE MBIO ZA TAIFA ZA NYIKA

Na  Dixon Busagaga was Globu ya Jamii Kanda ya kaskazini.

MWANARIADHA Failuna Abdi Matanga amefanikiwa kutetea nafasi yake ya kwanza katika mashindano ya Mbio za Taifa za Nyika zilizopewa jina la Ngorongoro National cross Country 2019 kwa upande wa wanawake baada ya kumaliza wa kwanza akitumia muda wa 34:55:99 .

Nafasi ya pili kwa upande wa wanawake ilichukuliwa na Mwanariadha Magdalena Shauri aliyetumia muda wa dakika 35:20:32 akifuatiwa na Angelina Tsere aliyeshika nafasi ya tatu akitumia muda wa dakika 36:45:83.

Kwa upande wa wanaume Mwanariadha  Faraja Damas amefanikiwa kushika nafasi ya kwanza baada ya kuhitimisha mbio akitumia muda wa dakika 30:17:19.

Nafasi ya pili kwa wanaume imechukuliwa na Joseph Panga aliyemaliza mbio akitumia muda wa dakika 30:29:37 na nafasi ya tatu kuchukuliwa na Marco Sylvester Monko aliyetumia muda wa dakika 30:29:36.


Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi Katibu mkuu was shirkisho la riadha Tanzania,Whilheam Gidabuday amesema mashindano hayo yalikua na lengo la kupata wanariadha watakaounda timu ya taifa itakayoshiriki mashindano ya Dunia ya mbio za nyika nchini Denmark mwezi ujao.
Wanariadha was mbio za Km 10 katika Mashindano ya Mbio za Taifa za Nyika wakianza kuondoka katika eneo la kuanzia Mbio hizo zilizo fanyika katika viwanja vya Moshi Club.

No comments: