Maksi za Mechi Ya Yanga vs Simba Uwanja wa Taifa

JANA, Yanga ikiwa wenyeji, ilifungwa na Simba bao 1-0 ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Hizi hapa ni takwimu za wachezaji waliocheza mechi hiyo ambayo Meddie Kagere ndiye aliyefunga bao hilo la ushindi kwa Simba dakika ya 71. upande wa kupandisha mashambulizi hakuwa vizuri. Dakika ya 23 alimchezea vibaya Paulo Godfrey na akaonyeshwa kadi ya njano.

Juuko Murshid – 7.0

Alikuwa mtulivu eneo la ulinzi wa kati. Ushirikiano wake mzuri na Pascal Wawa uliwafanya kuwa bora.

Pascal Wawa – 7.0

Kama ilivyo kwa Juuko, Wawa naye alikuwa kiongozi mkuu katika ulinzi. Alimfanya Makambo kushindwa kufurukuta.

James Kotei – 7.0

Bado anazidi kuwa bora siku hadi siku, Simba walionekana kuwa bora kati kutokana na utulivu wake.

Clatous Chama – 5.5

Kwa muda wa dakika 45 alizocheza kabla ya kutolewa na

YANGA Ramadhan Kabwili – 6.5

Hakupata mashambulizi mengi langoni mwake, alikuwa mtulivu kucheza mipira ya juu. Paulo Godfrey – 7.5 Aliipandisha Yanga na kuzuia mashambulizi. Krosi zake nyingi alizitendea haki lakini washambuliaji hawakuwa makini.

Gadiel Michael – 6.0

Alicheza kwa dakika 77 kisha akatolewa na kuingia Matheo Anthony. Kwa kiasi fulani alifanikiwa kuzuia mashambulizi kupita upande wake wa kushoto, lakini alishindwa kupandisha mashambulizi kwenda kwa wapinzani. Krosi zake nyingi hazikuwa na vipimo sahihi.

Andrew Vincent – 7.0

Kwa uwezo wake alifanikiwa kumzuia Meddie Kagere asilete hatari zaidi langoni kwao. Kosa moja alilolifanya la kuchelewa kumkaba ndilo likaigharimu Yanga wakafungwa.

Kelvin Yondani – 6.5

Alicheza vizuri. Alisaidiana na Andrew Vincent kuzuia mashambulizi. Dakika ya 81 alionyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea vibaya John Bocco.

Abdallah Shaibu – 7.5

Alicheza kwa uangalizi mkubwa sana na kupambana vilivyo na washambuliaji wa Simba pamoja na viungo wake.

Feisal Salum – 6.5

Kuna wakati alishindwa kuelewana na mwenzake Papy Tshishimbi. Lakini alifanikiwa kupambana na viungo wa Simba. Dakika ya 73 alimkwatua James Kotei, akaoneshwa kadi ya njano.

 

Papy Tshishimbi – 5.5

Hakucheza vizuri sana. Kwa muda wote wa dakika tisini alishindwa kuifanya safu yao ya ulinzi kuwa imara.

 

Heritier Makambo – 6.5

Alikosa msaada kutoka kwa mwenzake Amissi Tambwe, hata hivyo alipambana kwa kiasi fulani. Dakika ya 25 alipiga shuti lililomshughulisha Manula lakini likapaa juu.

 

Amissi Tambwe – 5.5

Alicheza dakika 45 pekee za kipindi kwanza, hakuwa na maajabu sana kwani mara kadhaa hakuwa akikaa kwenye eneo zuri la kushambulia hali iliyomfanya kutoka uwanjani bila ya kuisumbua safu ya ulinzi ya Simba. Dakika 45 alioneshwa kadi ya njano kutokana na kuushika mpira makusudi.

 

Ibrahim Ajibu – 6.0

Dakika 61 zilitosha kwake kuipambania Yanga ingawa hakubadilisha chochote mpaka anatolewa na kuingia Mohammed Issa. Alifanikiwa kupiga kona mbili na faulo mbili ambazo zilikuwa hatari langoni mwa Simba, lakini hazikuzaa matunda. Alishindwa kuipa presha zaidi safu ya ulinzi ya Simba ambayo muda mwingi ilionekana kucheza kwa uhuru
sana.

SIMBA

Aishi Manula – 6.0

Hakupata purukushani nyingi za kumpa shida. Alitulia sana, hakuwa na haraka.

 

Zana Coulibaly – 8.0

Krosi zake zaidi ya saba hatari ambazo hazikutumiwa vizuri na washambuliaji huku akionekana kuwa bora zaidi upande wake wa kulia, beki huyu raia wa Burkina
Faso alicheza vizuri katika nafasi yake. Aliwazuia Yanga wasicheze upande wake.

Mohammed Hussein – 6.0

Licha ya kutopewa mashambulizi mengi upande wake lakini yale mashambulizi machache aliyokabiliana nayo kwa kiasi fulani a l i – weza kuyadhibiti i n g a w a k w a kuingia Hassan Dilunga, kiungo huyu raia wa Zambia kwa kiasi fulani alifanikiwa kuichezesha timu, lakini wakati mwingine alichelewa kufanya maamuzi na kupoteza mipira.

 

Jonas Mkude – 7.0

Aliipandisha Simba, na kuwa wa kwanza kuzuia mashambulizi akishirikiana na Kotei. Ushirikiano wao mzuri unaendelea kuwa bora.

John Bocco – 7.5

Aliisumbua sana safu ya ulinzi ya Yanga. Ndiye aliyetoa pasi ya bao alilofunga Meddie Kagere dakika ya 71. Kwa kiasi kikubwa alikuwa chachu ya ushindi wa Simba.

Meddie Kagere – 8.0

Ndiye aliyeipa Simba ushindi kwa bao lake la dakika ya 71. Aliisumbua sana safu ya ulinzi ya Yanga, alikuwa mjanja wa kutokaa sehemu moja. Wakati anatoka dakika ya 90 na kuingia Haruna Niyonzima, alioneshwa kadi ya njano.

 

Emmanuel Okwi – 7.0

Alicheza kwa dakika 80 kisha akatolewa na kuingia Mzamiru Yasin. Alicheza vizuri, aliwasumbua walinzi wa Yanga hadi wakawa wanamchezea vibaya mara kwa mara. Dakika ya 58 alipiga shuti likagonga mwamba na kurudi uwanjani. Maksi za jana Taifa

Mrisho  Ngassa – 5.5

Mohammed Issa -5.0

Matheo Anthony – 4.5
Hassan Dilunga – 6.0

Mzamiru Yassin – 5.0

Haruna Niyonzima – 4.5

The post Maksi za Mechi Ya Yanga vs Simba Uwanja wa Taifa appeared first on Global Publishers.

No comments: