MAJALIWA AFUNGA SOKO LA WAKIMBIZI NA RAIA KIGOMA – VIDEO
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, ameamuru kufungwa kwa Soko la Nduta na kuagiza lihamishiwe ndani ya kambi ya wakimbizi ili kuhibiti wa Wakimbizi wanaotoka nje ya kambi kwa ajili ya kupata mahitaji kwani hawatakiwi kuchanganyika na raia.
Majaliwa amechukua hatua hiyo jana wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma kwenye Ukumbi wa Halmashauri hiyo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo na kuwataka watendaji wa halmashauri hiyo kumaliza haraka migogoro yao ya kiutendaji inayowakabili.
Waziri Mkuu ameamua kulifunga soko hilo la wakimbizi na wananchi wa kawaida baada ya soko hilo kubainika kuwa chanzo cha wakimbizi kutoka nje ya kambi kiholela na kushiriki katika kufanya matukio ya kiharifu.
Aidha, Majaliwa amemsimamisha kazi Mweka Hazina wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo, Thomas Chogolo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili za ubadhilifu wa makusanyo ya mapato ya halmashauri hiyo.
VIDEO: MSIKIE MAJALIWA HAPA AKIZUNGUMZA
The post MAJALIWA AFUNGA SOKO LA WAKIMBIZI NA RAIA KIGOMA – VIDEO appeared first on Global Publishers.
No comments: