BREAKING NYUZZZZ...... MALKIA WA TEMBO NA WENZAKE WAWILI WATIWA HATIANI KESI YA MENO YA TEMBO
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtia hatiani raia wa China, Yang Feng Glan (66) maarufu kama Malkia wa tembo, na wenzake Wawili baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi kumi na moja upande wa mashtaka Katika mashitaka ya kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh. bilioni 13, kinyume cha sheria.
Mbali na Feng washtakiwa wengine waliotiwa hatiani ni, wafanyabiashara raia wa Tanzania, Salvius Matembo na Philemon Manase, ambao wote walikuwa wakitetewa na mawakili Nehemia Nkoko na Hassan Kiangio.
Hukumu imeahirishwa baada ya dakika 30 ili washitakiwa wajitetee kabla ya kuhukumiwa.
Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.
No comments: