SHIRIKA LA WWF LAFANYA ZIARA KUFUATILIA MAENDELEO YA UTEKELEZAJI MRADI WA SECAD WILAYANI NAMTUMBO
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
SHIRIKA la Kimataifa la Hifadhi la World Wide Fund for Nature (WWF) limefanya ziara katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma kwa lengo la kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa mradi ujulikanao SECAD program ( Selous Eco-system Conservation and Development program).
SECAD ni mradi ambao kwa jumla utatekelezwa kwa miaka mitano ikiwa ni awamu ya kwanza na ya pili ambapo umejikita kuhakikisha wanaongeza uhifadhi wa mazingira kwa maana ya kwenye hifadhi ya Selous pamoja na ushoroba (corridor) unaounganisha pori la akiba la Selous na hifadhi ya Niassa ipatikanayo nchini Msumbiji
Mkuu wa Wilaya Namtumbo Sophia Kizigo jana kwamba ugeni wa shirika hili uliofika wilayani kwake ulitembelea na kujionea maendeleo ya mradi na kutembelea jumuiya ya uhifadhi ya Mbarang'andu ambapo walipata taarifa ya mradi na kujionea mafanikio, mipango na changamoto kwa sasa.
Mkuu wa Wilaya huyo ameueleza ugeni wa shirika hilo kuwa moja ya mafanikio ni mradi wa ufugaji wa nyuki kwa ajili ya kurina asali ambao unaosimamiwa na jumuiya hiyo pamoja na mpango wa ujenzi wa kiwanda cha kuongezea thamani asali pamoja na mabwawa ya samaki.
Kuhusu changamoto amesema moja ya changamoto ya mradi ni wananchi kuvamia maeneo ya hifadhi na kufanya shughuli za kibinadamu kama kilimo na ufugaji
Pia walitembelea Chuo cha Likuyu ambacho kinatumika kufundisha VGS (village scouts) wanaotumika kulinda hifadhi hizo.
Mkuu wa Wilaya Namtumbo Sophia Kizigo akipewa maelezo kuhusiana na maendeleo ya mradi wa wa SECAD program ( Selous Eco-system Conservation and Development program) wakati SHIRIKA la Kimataifa la Hifadhi la World Wide Fund for Nature (WWF) likifanya zaira wilayani yumo kufuatilia mradi huo
Eneo la mradi wa ufugaji wa nyuki kwa ajili ya kurina asali
Mkuu wa Wilaya Namtumbo Sophia Kizigo akiwa sambamba na Wadau wa SHIRIKA la Kimataifa la Hifadhi la World Wide Fund for Nature (WWF) wakionesha chupa ya asali ikiwa ni sehemu ya mafanikio ya mradi wa ufugaji wa nyuki kwa ajili ya kurina asali ,ambao unasimamiwa na jumuiya hiyo pamoja na mpango wa ujenzi wa kiwanda cha kuongezea thamani asali pamoja na mabwawa ya samaki.
Mkuu wa Wilaya Namtumbo Sophia Kizigo akikaribishwa mara baada ya kuwapokea wageni kutoka SHIRIKA la Kimataifa la Hifadhi la World Wide Fund for Nature (WWF) llilofanya ziara katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma kwa lengo la kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa mradi ujulikanao SECAD program ( Selous Eco-system Conservation and Development program).
No comments: