Mayweather Katika ‘Kickboxing’ na Mjapan Mwenye Miaka 20

BONDIA Floyd Mayweather Jr. anatarajiwa kupigana ‘kickboxing’ na Mjapan Tenshin Nasukawa (20) katika mkesha wa mwaka mpya nchini Japan. Bondia huyo alitangaza maamuzi yake hayo  baada ya kusaini mkataba na kampuni ya  Mixed Martial Arts (MMA) Promotions RIZIN Fighting Federation.

 

Mayweather hajawahi kupigana ndani ya  MMA na ratiba ya pambano hilo na  Nasukawa bado halijathibitishwa.

“Nilitaka kufanya kitu cha tofauti ,” alisema bingwa huyo mstaafu wa dunia wa uzito wa juu. “Nilitaka kuonyesha ujuzi wangu nje ya Marekani na niwe katika pambano maalumu.   Ninataka kuwapa watu kile wanataka — damu, jasho na machozi.”
Bondia huyo mwenye miaka 41 alisema taratibu na daraja la uzito vitathibitishwa ndani ya wiki chache zijazo.  Mabondia wote wawili wana rekodi nzuri katika michezo yao — Mayweather  ameshinda mapambano  50-0 bila kupoteza ilhali Nasukawa ameshinda 27-0  bila kupoteza ndani ya masumbwi na 4-0 ndani ya  MMA.

“Ni pambano kuu sana katika maisha yangu na ninataka kuwa mtu anayebadilisha historia.  Nitafanya hivyo kwa kutumia viganja vyangu hivi, kwa pigo moja tu — tazameni mtaona,” alisema Nasukawa.
Mayweather hajawahi kupigana pambano lolote tangu astaafu na kumpiga  Conor McGregor mwaka 2017  lakini amekuwa akihusishwa na mapambano kwa ajili pesa na mstaafu  Manny Pacquiao.
Katika mahojiano yake na  CNN’s Talk Asia hivi karibuni alisema, nafasi ya pambano lingine la marudiano na  Pacquiao  “ipo.”
“Tulipata nafasi ya kukutana ndani ya  Square Circle  na nilikuwa bora zaidi yake,” alisema.
Hivi karibuni aliitwa na rais wa UFC,  Dana White, ambaye alipendekeza bondia huyo afanye pambano na Mrusi Khabib Nurmagomedov. Taarifa za pambano dhidi ya chipukizi nyota wa Kijapan linaweza kuwa ishara mpya kwamba  Mayweather anafikiri  kuhamia ndani ya MMA.

The post Mayweather Katika ‘Kickboxing’ na Mjapan Mwenye Miaka 20 appeared first on Global Publishers.

No comments: