WHAAAT? MAISHA YA MREMBO WA DIAMOND YASHTUA
WHAAAT? Ndivyo unavyoweza kujiuliza ukiyajua kiuhalisia maisha ya baadhi ya mastaa wa Kibongo ukilinganisha na show-off zao. Baadhi ya wasanii Bongo hawapendi kuishi maisha yao halisi badala yake hujifanya kuwa na maisha fulani ya kitajiri ambayo hata robo yake hawajafikia. Kim Nana siyo jina geni kwenye Bongo Fleva ambapo kazi yake huwa ni kuuza sura (video queen) katika video za wasanii wa tasnia hiyo.
KIM NANA WA MONDI
Kim Nana ambaye jina lake halisi ni Lilian Kessy ni mrembo anayetikisa kwa sasa mitandaoni kwa kudaiwa kutoka kimapenzi na staa mkubwa wa Afro- Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ hivyo kupachikwa jina la Kim Nana wa Mondi.
Kama ni mfuatiliaji mzuri wa mitandao ya kijamii utakuwa umejionea ni kwa jinsi gani mrembo huyo amekuwa akiwika kwa kutupia picha kali, akiwa kwenye mandhari nzuri na magari ya kifahari.
Kufuatia maisha yake ya kujionesha, hivi karibuni watu wa karibu na majirani zake walibumburua mpango mzima wa maisha yake kwa Timu ya Operesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers.
ILIKUWAJE?
Ishu ilianza hivi, wakiwa kazini, OFM walipigiwa simu na mrembo mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Sweet Clara na kuanza kumwaga ubuyu.
“Hivi OFM mnajua kwamba huyu Kim Nana anafeki sana maisha? Yaani maisha anayoonesha mtandaoni siyo halisi kabisa, hata hizo nyumba anazopigia picha siyo anazoishi ni nyumba za jirani karibu na anapoishi. Sasa lengo la kuwapigia simu nataka mje muangalie wenyewe kwa macho yenu sehemu anayoishi maana hata majirani wanashangaa kwani haviendani kabisa na vitu anavyotupia mtandaoni,” alisema Sweet Clara na kuongeza:
“Unamuona na wigi la milioni moja na laki sita au gari la laki mbili na kiatu cha laki moja, lakini huku nyuma sehemu anayoishi ni majanga.”
KUMBE SIYO MBALI
Baada ya kunyetishiwa ubuyu huo na kuelekezwa anakoishi, OFM walifika eneo la nyumbani kwa Kim Nana na kugundua kwamba hapakuwa mbali na Ofisi za OFM (Global Publishers) kwa sababu walitumia dakika 15 kufika hapo.
OFM WAZAMA NDANI
OFM waligonga na kukaribishwa na kaka mmoja ambaye naye anaishi nyumba moja na Kim Nana.
Kaka: Karibuni.
OFM: Asante, samahani tuna shida na Kim Nana, tumesikia anaishi hapa.
Kaka: Kim Nana?
OFM: Ndiyo ila kwa jina lingine anaitwa Lilian.
Kaka: Ahaaa… ndiyo anaishi hapa, lakini tangu nimeamka sijaonana naye ila kuna muda nilimsikia anatoka, vipi mmempigia simu?
OFM: Ndiyo, lakini tangu tumeanza kumpigia hapokei ndiyo maana tukaona tuje hapa anapoishi.
Kaka: Mmh! Poleni, kama mtaweza kumsubiri msubirini anaishi kwa nyuma kwa sababu humu mna nyumba mbili, nyumba ya mbele ninaishi mimi alafu huko kwa nyuma ndiyo anaishi yeye.
OFM: Sawa tunashukuru ngoja tumsubiri. Wakati OFM ikimsubiri Kim Nana ilizunguka kwenye nyumba hiyo na kujionea mazingira yake ambayo yalionesha kuwepo kwa maisha ya uswahilini japokuwa siyo uswahilini.
Baadhi ya mambo yaliyoshtua ni pamoja na mazingira kuonekana machafu na jiko la gesi kuachwa nje likiwa na kutu likionesha kutofanyiwa usafi kwa muda mrefu. Ikiwa nyumbani hapo, OFM ilisogea mpaka mlangoni kwenye chumba kimoja cha Kim Nana ambapo iligonga mlango kwa muda mrefu bila mafanikio.
WAAMUA KURUDI KWA YULE KAKA
Baada ya kutoridhishwa na mazingira kisha kugonga bila mafanikio, OFM iliamua kurudi kwa yule kaka aliyewaelekeza awali ili kumuonyesha picha ya mrembo huyo kama ndiye wanayemtafuta au walimfananisha.
OFM: Kaka samahani tunakusumbua tena, hivi huyo Lilian ndiyo huyu (wanamuonesha picha ya Kim Nana) au tumekosea nyumba?
Kaka: Ndiyo, ndiye huyo Lilian, vipi kwani mmejaribu kugonga mlango?
OFM: Ndiyo, tumegonga mlango wa tatu tumeona kuna viatu nje, lakini hakuna mtu aliyetuitikia. Kaka: Kwani chumba anachoishi mnakijua?
OFM: Hapana, tulikuwa tunakisia tu.
Kaka: (anacheka) okey… chumba mlichokuwa mnagonga ndiyo hichohicho hamjakosea, endeleeni kumsubiri.
OFM iliendelea kumsubiria Kim Nana ambapo baada ya muda alifika dada mmoja na kuwasalimia OFM kisha akaenda kukaa mlangoni kwa Kim Nana naye alimsubiri kwa takriban dakika 20 na kuamua kumpigia simu akimfokea kuwa amemkalisha nje kwa muda mrefu na alimjulisha kuwa kuna watu walikuwa wanamsubiri (OFM).
Baada ya muda Kim Nana alifika na mtu aliyesemekana ni mtu wa karibu wa Diamond aliyetajwa kwa jina la Robby Platnumz ambaye alimleta Kim Nana na gari. Kim Nana alipofika aliwasalimia OFM na kuingia ndani na rafiki yake aliyejitambulisha kwa jina la Rehema Martin. “Baada ya kuona amekaa ndani kwa muda mrefu bila kutoka, OFM waliamua kugonga mlango, alipotoka walimwambia kuwa walitaka kufanya naye mazungumzo mafupi, lakini alikataa na kusema kwamba hayupo tayari kwa siku hiyo.
OFM: Lakini Kim Nana ni mazungumzo mafupi tu kwa sababu tumepigiwa simu na mtu anayekujua na akasema kwamba unafeki maisha mtandaoni, ndiyo maana tupo hapa tunataka kuongea na wewe.
Kim Nana: (anacheka) haaa… jamani, si nimeshawaambia siwezi kuzungumzia kitu chochote kwa sasa, tafadhali ninaomba mje siku nyingine.
Alipomaliza kusema hayo, Kim aliingia kwenye kichumba chake kimoja na kufunga mlango, OFM nao wakaona isiwe ishu wakaamua kuondoka na kurudi ofisini baada ya kukaa pale kwa takriban saa tatu (kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 9:00 alasiri).
Mwanangu bado ni mbaya kila baada ya wiki mbili au moja anatakiwa aende hospitali za hapa nchini kwa ajili ya kutolewa maji kwenye tumbo lake na gharama zote natoa mwenyewe, nawaomba Watanzania wenzangu wasichoke kunisaidia, waendelee kumchangia Hawa ili naye apate nafuu,” alisema Mama Hawa.
Hata hivyo, Ijumaa liliamua kumtafuta mlezi wa hawa Pili Misanah hili kutaka kujua kama ana taarifa za kusafiri Kwa Hawa. “Kwa kweli sifahamu Hawa atasafiri lini kwenda nje kimatibabu, ila ninachojua visa na pasipoti vyote vipo tayari sasa sijaelewa kwa nini mpaka sasa hivi bado Hawa hajaenda kwenye matibabu, labda naomba mtafute Babu Tale ndiyo anajua kila kitu na anaweza akawaambia ishu nzima ikoje,” alisema Pili.
Babu Tale alipoulizwa kuhusu ishu hiyo alisema kwamba wao wameshaanda kila kitu kipo tayari hivyo wiki hii wapo mbioni kusafiri. “Tumeshaandaa kila kitu kipo tayari tunasubiri tu ruhusa ya matibabu (Referral) kutoka Muhimbili ndio tupange siku ya kuondoka, nadhani ndani ya wiki hii hii tunaweza kuondoka,” alisema Babu Tale. Mama Hawa ameomba Watanzania kuendelea kumsaidia mwanaye kupitia namba 0712 032705 au 0762 313587.
The post WHAAAT? MAISHA YA MREMBO WA DIAMOND YASHTUA appeared first on Global Publishers.
No comments: